Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini imelitaka Jeshi la Polisi Nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za jeshi ilo ili kuepuka vitendo vya uvunjifu wa haki za Binadamu.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu, Mathew Mwaimu wakati akitoa taarifa ya Tathmini kuhusu mwenendo na utendakazi wa Jeshi ilo nchini kwaanzia mwaka 2020 hadi 2022.
Mwaimu amesema tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ilifanya uchunguzi kumi ikiwemo kutembelea vituo vya polisi katika baadhi ya mikoa nchini na kubaini kupigwa na kuteswa kwa watuhumiwa wakati Ukamataji au wakati wa upelelezi,kuwepo tuhuma za Rushwa dhidi ya baadhi ya Askari.
Pia Jaji Mwaimu amesema tume hiyo imebaini baadhi ya Askari polisi kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu vitendo wanavyolalamikiwa na wananchi pamoja na watuhumiwa kuwekwa mahabusu za polisi muda mrefu bila dhamana.
Aidha,Jaji Mwaimu amelitaka jeshi la polisi kuzingatia sheria ya Jeshi la polisi na huduma saidizi sura ya 322,sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai sura 20 na kanuni za jeshi la polisi za mwaka 2013 ambazo zimeainisha kazi za jeshi ilo
No comments:
Post a Comment