Friday, June 24, 2022

Mapendekezo Manne ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwenye Suala la Katiba Mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Wakili Anna Henga akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo mkoani Dar es salaam.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetangaza mapendekezo manne kufatia kauli ya chama cha Mapinduzi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri kuu ya chama hicho  kuwa imeridhia kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga amesema kauli ya chama hicho kikongwe kuridhia kuanza kwa mchakato huo ni ya kupongezwa.

Alisema LHRC inapendekeza Serikali kuanza kwa kupeleke mswada wa katiba, mswada wa sheria, pamoja na rasimu ya pili ya Katiba pendekezwa (katiba ya Warioba) kisha ianze majadiliano na wananchi kupitia mikutano hata vyombo vya habari.

“Ikumbukwe kuwa 31 Disemba 2010 aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa Katiba katika kongamano la LHRC ambalo lilibeba kauli mbiu ya KATIBA MPYA NI WAJIBU” Alibainisha Wakili Henga.

Kwa upande wake Afisa programu wa LHRC bwana  Maduhu William aliongezea kuwa mchakato wa Katiba ni jumuishi hivyo kuna watu wa makundi mbalimbali basi uwe shirikishi kwa watu wote.

“Katiba ni zaidi ya Dola, ili mchakato uwe hai lazima uwe rafiki ushirikishe makundi yote wakiwemo walemavu, wazee, vijana, wanafunzi kwa kufanya hivyo mchakato utakuwa rafiki kwa makundi yote ” Alisema Bw. Maduhu 

No comments: