Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akipokea Baraka kutoka kwa Mhashamu Baba askofu Simon Masondole, askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda mkoani Mara wakati wa ibada ya ufunguzi wa kanisa katoliki Kigango cha Muliaza Parokia ya Butiama leo 03/07/2022. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi
Mhashamu Baba askofu Simon Masondole askofu wa jimbo katoliki la Bunda amepongeza kitendo cha kizalendo cha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, kwa kuwa mzalendo na kuchangia maendeleo kwa kujenga kanisa kitendo ambacho kitakuwa daraja litakalowezesha kuvusha wengine katika kuufikia wokovu.
Askofu Masondole amesema hayo Musoma Mkoani Mara wakati akiongoza ibada ya Misa takatifu iliyoambatana na ufunguzi wa kanisa kigango cha Muliaza parokia ya Butiama, kanisa ambalo limejengwa kupitia uwezeshaji wa IGP Sirro, wadau pamoja na watu wengine waliofanikisha ujenzi wa kanisa hilo.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewapongeza wadau mbalimbali walioshirikiana nae hadi kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo ambapo pia amewataka watu wengine kuendelea kukumbuka mazingira ya nyumbani kwao wanakotoka kwa kusaidia jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment