Friday, August 19, 2022

NSSF yajipanga kukusanya Trioni 7.3 katika Mwaka wa fedha 2022/2023

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umepanga kukusanya kiasi Cha shilingi trioni 7.3 katika Mwaka wa fedha 2022 / 2023 Kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Masha Mshomba akiongea na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti, 19 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa huo Bw. Masha Mshomba, alipokua akizungumza na waandishi wa habari, akitoa Taarifa ya Utendaji wa Mfuko pamoja na Vipaumbele vya Mfuko kwa mwaka wa Fedha  2022/23.

Amesema kuwa, ukuaji huo ni mkubwa tofauti na miaka miwili ya nyuma iliyopita ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa ni Shilingi Trilioni 4.3 na kuwa ukuaji huo umechangiwa na ongezeko la makusanyo ya michango.

"Tumepata mafanikio makubwa katika suala zima la ukuaji wa Mfuko na hii imesababishwa na sababu kadhaa ikiwemo kuweka misingi imara na madhubuti ya ukusanyaji wa mapato" amesema Mshomba.

Ameongeza kuwa, katika mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022, Mfuko ulikusanya zaidi ya Shilingi Trilioni 1.42 kwamba makusanyo hayo ni zaidi ya hata bajeti ambayo walijipangia iliyokuwa Shilingi Trilioni 1.38, ambapo pia Mfuko umeboreshaji sana udhibiti wa matumizi jambo ambalo limechangia ukuaji wa NSSF.

Amesema kuwa, mafanikio mengine yaliyopatikana, ni pamoja na uboreshaji wa huduma hasa kwa kutumia mifumo mbalimai ya TEHAMA ambapo sasa mwanachama na wadau wanaweza kupata huduma popote walipo bila ya kufika katika ofisi za NSSF kwa kutumia mifumo ya waajiri na wanachama yaani Employer Potal na Member Potal.

Mshomba alisema Mfuko pia unapata matokeo mazuri sana katika Uwekezaji hasa ukizingatia kuwa wanawekeza katika maeneo salama ambapo katika kipindi cha miaka miwili uwekezaji umeleta mapato makubwa.

"Ilikuwa haijafikiwa NSSF kuweza kupata mapato ya mwaka zaidi ya Shilingi bilioni 500 lakini katika mwaka huu wa fedha umepata zaidi ya Shilingi bilioni 600,matokeo haya ya uwekezaji yametokana na Mfuko kujikita zaidi katika uwekezaji kwenye maeneo ambayo yanaleta faida kwa Mfuko na kuhakikisha wanaudhibiti wa fedha"amesema Mshomba.

Hata hivyo, amesema chachu kubwa ya mafanikio ya NSSF imechagizwa na kasi ya utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu amekuwa chachu ya ongezeko kubwa la wawekezaji hapa nchini hususan katika sekta binafsi kutokana na kufungua fursa za uwekezaji.

Kuhusu waajiri kutowasilisha michango alisema wameweka mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ili kupata orodha kamili ya waajiri ambao watawafikia na kufuatilia michango ya wanachama.

Mshomba aliwahamasisha Watanzania wote kushiriki katika zoezi zima la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo tarehe 23 Agosti, 2022 ili waweze kuhesabiwa.

Thursday, August 18, 2022

Wiki ya AZAKI Kuzinduliwa leo Agost 18, 2022 jijini Dar es salaam

Na vicent Macha Dar es salaam.

Sekta binafsi zimetakiwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (AZAKI,) Ili kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili Jamii kwa kuwafikia wananchi kufahamu mahitaji yao na kuyapatia ufumbuzina kuleta maendeleo ya ya Taifa kwa ujumla.

Zoezi la Uzinduzi wa wiki ya Azaki likiendelea mapema leo jijini Dar es salaam.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati akifungua wiki ya AZAKI inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Oktoba mwaka huu.

Aliyaongea hayo leo Agosti 18 jijini Dar es Salaam ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maendeleo ya Watu, Habari Fanikiwa za Watu” na Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika jijini Arusha.

Aidha Nsekela amesema kuwa matokeo chanya yatapatikana kupitia wiki ya AZAKI na inaonekana dhahiri tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018 licha ya changamoto lakini kumekua na kuongezeka kwa umoja na mshikamano miongoni mwa wadau.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela.

‘’Suluhisho ya changamoto zinazoikumba jamii yetu inahitaji ushirikiano baina ya wadau ikiwemo mashirika, taasisi, sekta binafsi, Asasi za kiraia na Serikali kwa ujumla, ushirikiano na AZAKI na sekta binafsi ni hafifu tukishirikiana tutafika mbali zaidi katika kujenga uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla.’’ Amesema. Nsekela

Sanjari na hayo Mkurugenzi amesema, Ushirikiano baina ya AZAKI na sekta binafsi utasaidia kutatua changamoto kwa kiasi kikubwa kuwafikia wananchi wengi zaidi mjini na vijijini.

Nsekela amewasisitiza washiriki hao kuainisha njia mbalimbali mpya za kuwafikia wananchi na maendeleo kwa kuzingatia ushirikiano baina ya AZAKI hizo na sekta binafsi hasa katika uwekezaji utakayosaidia kuzalosha ajira

‘’Tujadili uwekezaji wa manufaa ya kiuchumi na kuwapa watanzania utulivu wa kiuchumi kwa kutoa wigo kwa ushirikiano baina ya sekta binafsi na AZAKI katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na sekta nyingine za uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS,) Bw. Francis Kiwanga amesema katika wiki hiyo ya AZAKI wanataraji matokeo chanya hasa katika kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali, sekta binafsi na Asasi za kiraia katika ujenzi wa Taifa na ushiriki wa wananchi katika kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC,) Anna Henga amesema kusanyiko hilo la wana AZAKI tangu kuanza kwakwe 2018 limekuwa na malengo ya kufikia maendeleo endelevu pamoja na kubadili mtazamo wa wananchi na kutambua mchango wa Asasi za kiraia.

Hata hivyo amesema ni muhimu sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika wiki hiyo muhimu hasa katika kupanua wigo wa kuwafikia wananchi, kutambua changamto za na kuzipatia suluhu na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuonesha ushirikiano tangu kuanzishwa kwa kusanyiko la Asasi za kiraia mwaka 2018.

Amesema, wiki ya AZAKI kwa mwaka 2022 itakuwa tofauti na licha ya kueleza mafanikio na maendeleo yaliyofikiwa wana AZAKI watatawanyika katika maeneo mbalimbali, kukutana na wananchi na kueleza huduma ambazo AZAKI zinatoa kwa wananchi.

Wednesday, August 17, 2022

Watanzania wahamasishwa kuchangamkia fursa ya Uwekezaji na

Na Vicent Macha, Dar es salaam

Kituo Cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) imewaomba Watanzania ambao wana nia ya kufanya Uwekezaji katika sekta mbalimbali, wachangamkie  fursa hizo nasio kuwachia wawekezaji kutoka mataifa mengine  kuja kuwekeza hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) Jonh Mnali.

Rai hiyo imetolewe na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho Jonh Mnali wakati akizungumza na  Waandishi wa habari Kuhusu Mafanikio ya TIC katika kipindi Cha Mwaka 2021/ 2022,ambapo amebainisha kuwa watananzani bado hawajitokezi kuwekeza katika fursa  mbalimbali za Uwekezaji zilizopo.

" Naomba kutoa wito kwa watanzania wajitokeze kuchangamkia fursa za Uwekezaji katika maeneo yao,waondokane na dhana ya kufikiria kwamba Uwekezaji unawahusu watu kutoka nje ya nchi pekee,bali watambue uwekezaji unawahusu wawekezaji wa ndani na nje ya nchi" amesisitiza Mnali

Amendelea kusema kuwa TIC imefanikisha Uwekezaji kwa kufanya maboresho ya kituo Cha utoaji wa huduma za mahali pamoja " One Stop Facilitation Centre ya TIC" nakwamba taasisi zipatazo 12 za  serikali kwa sasa zinatoa huduma katika kituo cha mahali pamoja ambapo taasisi hizo ni Wizara ya Kazi,Wizara ya Ardhi,Uhamiaji,NIDA,NEMC,TRA,BRELA,TBS,TMDA,OSHA, TANESCO pamoja na TIC wenyewe.

Amesema kuwa TIC inaendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje kwa kushirikiana na ofisi za kibalozi na ofisi za wakuu wa Mikoa, ambapo TIC inaendelea kupokea wawekezaji wenye nia ya kuwekeza nchini,hatua hiyo ni kutokana na serikali  kuendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Ujenzi wa Miundombinu wezeshi kama vile barabara,reli,bandari,viwanja vya ndege na umeme.

" Katika kipindi cha kuanzia Juni 2021 hadi 2022 uhamasishaji uwekezaji wa nje umeendelea kufanyika kupitia makongamano ya uwekezaji yaliyofanyika Qatar,Doha na ushiriki wa TIC kwenye kongamano na maonesho haya yameleta matokeo chanya ambapo wawekezaji mbalimbali walifika nchini kukutana na wataalamu wa sekta ambazo wanahitaji zaidi kuwekeza" amesema Mnali.

Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TIC ameongeza kuwa wawekezaji wa ndani wameendelea kutembelea kituo cha Uwekezaji kutafuta fursa ,huku TIC pia imeendelea kusaidia wawekezaji hao kuratibu uwasilishwaji wa miradi ya watanzania katika majukwa mbalimbali yanayohusu uwekezaj.

Hata hivyo amefafanua kwamba Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha inarahisisha utoaji huduma kwa kuondoa urasmu ,kutumia teknolojia ya mawasiliano ,na kuweka vigezo vinavyotumika kutoa huduma Kama vile cheti cha uwekezaji ambacho kimefanya uboreshaji ya utendaji kazi wa ndani,mtirirko was nyaraka na mafaili,utoaji maamuzi wenye tija,pamoja na kuweka vigezo na viwango vya utoaji huduma kwa wawekezaji.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Jonh Mnali, amesema kipindi cha mwezi Juni 2021 hadi 2022 jumla ya miradi 274 imesajiliwa ikilinganishwa na miradi 234 iliyosajiliwa katika kipindi hicho Mwaka 2020/ 2021 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.6 ,miradi iliyosajiliwa katika kipindi hicho inatarajiwa kuzalisha ajira 43,925 ukilinganisha na ajira 36,470 zilizoripotiwa kipindi hicho mwaka 2020/ 2021.

Tuesday, August 16, 2022

TRA Kukusanya Shilingi Trilioni 23.65, Mwaka wa fedha 2022/2023

 

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari Leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa makusanyo ya Kodi mwaka 2022/23.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo, amesema mamlaka hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/2023, inatarajia kukusanya Shilingi Trilioni 23.65, ikiwa ni sehemu ya bajeti kuu ya Serikali ya Shilingi Trilioni 41.48, ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2021/2022, walikusanya kiasi cha shilingi Trilioni 22.99.

Bw. Kayombo amesema kufuatia ongezeko la makadirio ya makusanyo hayo, TRA inaendelea kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wafanyakazi na wafanyabiashara, ya kuhusu sheria mbalimbali za kodi, tozo na ada zilizofanyiwa marekebisho ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa sawa na kurahisisha ukusanyaji na ulipaji kodi kwa hiari na kutimiza majukumu na malengo yaliyowekwa katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amewataka watanzania kulipa kodi inavyostahili ili kujenga uchumi wa nchi.

*“Katika mwaka wa Fedha 2022/2023 tumeanza kwa kasi ya kuelimisha watumishi wetu na wafanyabiashara kote nchini juu ya mabadiliko mbalimbali ya sheria mbalimbali za kodi, tozo na ada zinazosimamiwa na TRA pamoja na taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya Serikali.”* Amesema Bw. Kayombo.

Aidha amebainisha kuwa, marekebisho na mabadiliko ya sheria za kodi yamefanyika kwa lengo la kuongeza kasi ya kufufua uchumi na kuimarisha sekta za uzalishaji kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi, ambapo miongoni mwa mabadiliko ni pamoja na sheria ya usimamizi wa kodi ambayo inamtaka kila mwananchi mwenye Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

“Katika mabadiliko ya sheria ya usimamizi wa kodi, Sheria ya sasa inamtaka kila Mwananchi mwenye Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kusajiliwa na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ili kumwezesha katika shughuli zake za kila siku”.* Amesema Bw. Kayombo.

Amesema katika mwaka wa fedha uliopita wa 2021/2022, Mamlaka hiyo ilifanikiwa kutatua changamoto za walipakodi, kuweka mazingira mazuri ya kulipa kodi, kuongeza kasi ya kusajili walipakodi wapya, kuwekeza kwenye TEHAMA na kutoa elimu na kuhamasisha

Ripoti ya ya wafanyabishara wa Mipakani yazinduliwa leo jijini Dar es salaam.

Liberty sparks ni Shirika lisilo la Kiserikali, lilojikita katika elimu na tafiti, linalotekeleza mradi wa urahisi wa kufanya biashara nchini Tanzania ambao unafadhiliwa na taasisi ya Atlas Network”.

Mradi huu unategemea kuleta maboresho katika mazingira ya biashara kwa kutazama uboreshaji viashiria vya kiuchumi vinavyo tolewa na riport mbalimbali ikiwemo Ripoti ya Benki kuu ya dunia mwaka 2020. 

Mradi huu chini ya kampeni ya Ujirani mwema ,ambapo hapa tuna angaliautaratibu, muda na gharama katika utumaji na uingizaji wa bidhaa mipakani kwa kuzingatia muda,taratibu na gharama zilizowekwa kisheria.

Kama think tank, tumegundua sehemu ya biashara za mipakani kwa sasa Tanzania imekuwa haifanyi vizuri sana ukilinganisha na nchi nyingine zilizopo chini ya Jangwa la Sahara kama Mauritius, Rwanda, Kenya, Botswana, Burundi na nchi nyinginezo katika urahisi wa kufanya biashara.

Ingawa Tanzania ilipanda kwa ngazi tatu kwenye ripoti ya benki kuu ya dunia mwaka 2019 -2020 bado kuna huitaji mkubwa wa kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi, hili litatusaidia kutangaza na kuvutia wawekezaji nchini na kuwezesha vijana wetu kujiajiri wanapomaliza vyuo vikuu.

Naibu waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda Exaud Kigahe akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Wafanyabisahara wa Mipakani Mapema leo jijini Dar es salaam.

Liberty sparks inatambua mchango mkubwa wa serikali wa kuboresha mazingira rahisi na rafiki ya ufanyaji biashara pamoja na kutambua mchango mkubwa wa wadau katika kuchochea maendeleo ya nchi,na kutoa nafasi ya kufanya tathmini ya vipaumbele vya sera kwa kulinganisha na nchi na chumi zilizofanikiwa duniani kwa kuwa na mazingira bora ya ufanyaji biashara za mipakani na ukuaji wa uchumi katika kupambana na umaskini.

Katika kampeni hii tumefanikiwa kufanya tafiti ilayofanywa na Daktari Sauti Magai kutoka (College of Business) chuo kikuu cha Dar es Salaam. Tafiti hii inalenga kuboresha biashara za mipaka kama nilivyosema awali kwa kuzingatia taratibu,muda na gharama.

Sasa ili kufikia malengo hayo, tumeita wadau kutoka sekta binafsi pamoja na serikali na kuunda kikosi kazi kilichotoa mapendekezo ya pamoja kwa kuzingatia utendaji na uwakilishwaji wa moja kwa moja. 

Ni mategemeo yetu kupitia ripoti hii iliyotolewa leo na mgeni rasmi kuwa Mh Exaud Kigahe yataumika katika kufanya maboresho ya kisera na kuweka mazingira bora na rafiki yaufanyaji biashara Tanzania.

Tunaamini kwamba kila mtanzania akipata nafasi na kuweza kufanya biashara kwa urahisi, tutaweza kabisa kupunguza tatizo la umasikini na ajira kwenye kaya zetu kwa sehemu kubwa.

Hili litasaidia kuchochea maendeleo ya jumla na kuondokana na utegemezi. Hatua hii ya kuwaleta serikali na sekta binafsi kwa pamoja itasaidia kutoa mapendekezo yenye mchango chanya kwenye mpango wa muda mrefu wa Tanzania (TDV 2025), Mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2021/2022 - 2025/2026) na maendeleo endelevu ya Dunia 2030.

Wadau walioshiriki leo ni kutoka serikalini na sekta binafsi ni kama wafuatao; 

Ni matengemeo yetu Taasisi za kiserikali , waandishi wa habari, wabunge, wanazuoni na wadau wengieneo wa maendeleo watatuunga mkono katika kampeni hii ya kuboresha mazingira ya biashara Tanzania.

Matokeo ya mda mrefu na mfupi ya mradi huu ni kuona mazingira ya biashara yakichochea maendeleo ya nchi na watu kwa pamoja.

Baadhi ya Wajumbe wakufuatilia matukio yanayoendelea katika Uzinduzi wa ripoti ya Wafanyabiashara wa Mipakani.