Wednesday, August 17, 2022

Watanzania wahamasishwa kuchangamkia fursa ya Uwekezaji na

Na Vicent Macha, Dar es salaam

Kituo Cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) imewaomba Watanzania ambao wana nia ya kufanya Uwekezaji katika sekta mbalimbali, wachangamkie  fursa hizo nasio kuwachia wawekezaji kutoka mataifa mengine  kuja kuwekeza hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) Jonh Mnali.

Rai hiyo imetolewe na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho Jonh Mnali wakati akizungumza na  Waandishi wa habari Kuhusu Mafanikio ya TIC katika kipindi Cha Mwaka 2021/ 2022,ambapo amebainisha kuwa watananzani bado hawajitokezi kuwekeza katika fursa  mbalimbali za Uwekezaji zilizopo.

" Naomba kutoa wito kwa watanzania wajitokeze kuchangamkia fursa za Uwekezaji katika maeneo yao,waondokane na dhana ya kufikiria kwamba Uwekezaji unawahusu watu kutoka nje ya nchi pekee,bali watambue uwekezaji unawahusu wawekezaji wa ndani na nje ya nchi" amesisitiza Mnali

Amendelea kusema kuwa TIC imefanikisha Uwekezaji kwa kufanya maboresho ya kituo Cha utoaji wa huduma za mahali pamoja " One Stop Facilitation Centre ya TIC" nakwamba taasisi zipatazo 12 za  serikali kwa sasa zinatoa huduma katika kituo cha mahali pamoja ambapo taasisi hizo ni Wizara ya Kazi,Wizara ya Ardhi,Uhamiaji,NIDA,NEMC,TRA,BRELA,TBS,TMDA,OSHA, TANESCO pamoja na TIC wenyewe.

Amesema kuwa TIC inaendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje kwa kushirikiana na ofisi za kibalozi na ofisi za wakuu wa Mikoa, ambapo TIC inaendelea kupokea wawekezaji wenye nia ya kuwekeza nchini,hatua hiyo ni kutokana na serikali  kuendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Ujenzi wa Miundombinu wezeshi kama vile barabara,reli,bandari,viwanja vya ndege na umeme.

" Katika kipindi cha kuanzia Juni 2021 hadi 2022 uhamasishaji uwekezaji wa nje umeendelea kufanyika kupitia makongamano ya uwekezaji yaliyofanyika Qatar,Doha na ushiriki wa TIC kwenye kongamano na maonesho haya yameleta matokeo chanya ambapo wawekezaji mbalimbali walifika nchini kukutana na wataalamu wa sekta ambazo wanahitaji zaidi kuwekeza" amesema Mnali.

Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TIC ameongeza kuwa wawekezaji wa ndani wameendelea kutembelea kituo cha Uwekezaji kutafuta fursa ,huku TIC pia imeendelea kusaidia wawekezaji hao kuratibu uwasilishwaji wa miradi ya watanzania katika majukwa mbalimbali yanayohusu uwekezaj.

Hata hivyo amefafanua kwamba Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha inarahisisha utoaji huduma kwa kuondoa urasmu ,kutumia teknolojia ya mawasiliano ,na kuweka vigezo vinavyotumika kutoa huduma Kama vile cheti cha uwekezaji ambacho kimefanya uboreshaji ya utendaji kazi wa ndani,mtirirko was nyaraka na mafaili,utoaji maamuzi wenye tija,pamoja na kuweka vigezo na viwango vya utoaji huduma kwa wawekezaji.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Jonh Mnali, amesema kipindi cha mwezi Juni 2021 hadi 2022 jumla ya miradi 274 imesajiliwa ikilinganishwa na miradi 234 iliyosajiliwa katika kipindi hicho Mwaka 2020/ 2021 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.6 ,miradi iliyosajiliwa katika kipindi hicho inatarajiwa kuzalisha ajira 43,925 ukilinganisha na ajira 36,470 zilizoripotiwa kipindi hicho mwaka 2020/ 2021.

No comments: