Tuesday, October 30, 2012

KOVA ASTUKIA MAANDAMANO YANAYOANDALIWA NA WAISLAM.asema wanaaanza kuwasaka wote



POLISI nchini wamepanga kusambaratisha mtandao unaodhamini na kuchapisha vipeperushi vinavyohamasisha kufanyika kwa maandamano, kutaka kutolewa kwa Katibu wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda  Issa Ponda na wenzake.
  

        Hatua hiyo imekuja baada ya waumini hao kupanga kufanya maandamano  Novemba Mosi, ambayo yatahamasisha mahakama hiyo kutoa dhamana kwa kiongozi wa taasisi hiyo na wenzake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema wataanza kufanya msako wa wote wanaohamasisha, wanaochapisha na wanaotoa vipeperushi ili kuwakamata.
“Tunafuatilia wadhamini na wachapishaji wa vipeperushi kwani ni chanzo cha uchochezi na upotevu wa amani nchini,” alisema Kova.
    

Kova alisema maandamano hayo ambayo yamepangwa na waumini hao yanatishia amani , wananchi watashindwa kwenda kazini na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Monday, October 29, 2012

Utajiri wa Kamanda Barlow waanikwa

 

 

         SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa yake ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, umeibuka utata wa mali alizokuwa akimiliki, huku akidaiwa kumiliki utajiri wa kutisha likiwamo jengo la ghorofa.

Habari za kiuchunguzi zilizopatikana zinaeleza kuwa mbali ya jengo hilo, Kamanda Barlow anadaiwa pia kumiliki magari zaidi ya saba yakiwamo malori mawili aina ya Fuso, malori mawili ya mchanga, gari dogo aina ya Toyota Cresta pamoja na Toyota Hilux Double Cabin.

Magari hayo yanadaiwa kuhifadhiwa eneo la Nyakato mjini Mwanza, yakisimamiwa na mfanyabiashara mmoja kwa niaba yake.

Mbali na magari hayo kamanda hyo anatajwa kumiliki nyumba ya kifahari mkoani Mara, ambayo aliijenga alipokuwa RPC mkoani humo, huku nyumba nyingine ikiwa maeneo ya Capri-Point jirani na Ikulu ndogo mkoani Mwanza, inayoelezwa kuwa aliinunua baada ya Serikali kutangaza uuzaji wa nyumba zake kwa watumishi wake.

Umiliki wa mali hizo umeibua maswali mengi, wengi wakitaka kujua iwapo zinalingana na kipato cha Kamanda Barlow, licha ya kuwa na cheo cha Kamanda wa Polisi wa mkoa.

VIGOGO 10 WATAJWA KUHUSIKA NA KUFICHA HELA USWISI

VIGOGO 10 wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.
Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).
Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).

              Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.
Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: “Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge.”
“Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?.”
        Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.
“Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi,” alisema Zitto.
Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.

    Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.
Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.
       

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.

Thursday, October 25, 2012

MWALIMU WA TLC ASEMA HAWAKO TAYARI KUWAONGEZEA WANAFUNZI SIKU ZA KUSOMA

 



asisitiza wasiokuwa na gazeti tando (blog)ita kula kwao.

    >awasifu  wanafunzi kwa kuonyesha nidhamu kwa kipindi chote cha mafunzo..

Mara baada ya uvumi uliokuwa ukisambazwa  na baadhi ya wanafunzi, wanaopata mafunzo kwa vitendo katika kituo cha mafunzo kwa vitendo( TLC). Uvumi huo  umepingwa  vikali na mmoja wa viongozi wa kituo hicho kwa kubainisha kuwa hawafikirii, na hawana mawazo ya kuongeza muda kwa madai kuwa wao wanafanya kazi kwa kufata ratiba ya utendaji kazi wa kituo hicho.

Akizungumza na mwandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es salaam, meneja biashara wa kituo hicho Bw. Dastan Kamanzi  alisema kuwa uvumi huo hauna chembe hata moja ya ukweli, kwa kuwa wao wanafanya kazi kwa kufuata ratiba ya kituo hicho” swala hilo la kuongeza muda halina ukweli wowote kwa sababu tunafata ratiba na tunakazi  nyingi za kufanya pia muda uliokuwa umepangwa umekwisha na tutakuwa na kazi ya  kuandaa matokeo ya wanafunzi “alisema kamanzi.na kuongeza kuwa wao hawana lengo la kumfelisha  mtu bali haki itatendeka kwa kila kazi iliyofanywa na mwanafunzi.

Akizidi kufafanua kwa undani zaidi  jinsi mafunzo yalivyoendeshwa kwa kipindi   cha miezi mitatu, kamanzi alisema  kuwa wamefundisha kila kitu ambacho walitakiwa kukifundisha  hivyo hakuna mada iliyoachwa kwani wao wanafundisha kwa kufuata mtaala, “kila mwalimu amefundisha mada zote kama inavyotakiwa. Akitolea  mfano kwenye somo la new media kila mwanafunzi  kafundishwa jinsi ya kufungua blog, sasa kuna haja gani ya kuongeza muda wakati kila kitu kimefundishwa” alisema kamanzi, pia alikemea tabia ya wanafunzi wanaofungua blog kwa lengo la kupata alama pasipo kujua kuwa zina faida kubwa kwao kama wakiziendeleza“ kuna wanafunzi wakisha sahihishiwa na kupewa alama zile blog zao wanaziacha hivyo si vizuri kwani  blog wakiziendeleza  wanaweza kujipatia kipato kwa kuweka matangazo ya watu mbalimbali  lakini wao hawalijui hilo” aliongeza kamanzi.

Akiendelea kutoa ufafanuzi kwa undani zaidi na jinsi wanavyopata  changamoto walizokutana nazo Bw. Kamanzi alisema kuwa darasa la awamu hii halikuwa na matatizo, kama ya awamu iliyopita kutokana na wanafunzi kuwa na nidhamu ya hari ya juu. Na kutolea mfano suala  la wizi na kugombana matatizo ambayo yalijitokeza katika awamu iliyopita, pia alitoa wito kwa wanafunzi wasio kuwa na brog kuwa nazo kwani kutokuwa nazo kutawapunguzia alama na  kuwataka wanafunzi ambao hawajamaliza kazi zao kukamilisha na kuzipeleka kwa walimu husika.

Nae mwanafunzi  wa kituo hicho Exuad Mtei alisema kuwa uvumi huo haukumuathili  kitu chochote kitaaluma kwa kuwa hadaiwi kazi yoyote na mwalimu” mimi waongeze muda  wasiongeze sina shida kazi kwao ambao kawajamaliza kazi za walimu wao. Pia naunga mkono kauli ya kutoongeza mda kwa sababu hata mimi nina shughuli zangu za msingi  nahitaji  kuzifanya wakiongeza muda wataniharibia ratiba” alisema Bw. Mtei, huku baadhi ya wanafunzi  wakikataa kulizumngumzia suala hilo.

Kituo cha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari TIME (TSJ) kilianzishwa  mnamo mwaka  2010, chini ya udhamini wa mwaka mmoja kutoka Tanzania Media Fund ( TMF).Nia na Madhumuni  na lengo la kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo. Katika Nyanja mbalimbali za Utangazaji,kama vile Radio, Television production, Printing na photo journalism kwa wanafunzi wa Stashada ya nne.   

 

MULUGO AOMBA RADHI KWA YALIYOTOKEA

Siku chache mara baada ya Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi  Philipo Mulugo kudaiwa  kubolonga alipokuwa akiwasilisha hotuba yake katika mkutano  wa kimataifa kwa kuonyesha mbele ya jamii ya kimataifa kuwa haijui historia ya nchi yake naibu huyo amewaomba radhi watanzania.

Akizungumza katika kipindi cha power break fast kinachorushwa  na kituo cha redio clous cha jijini Dar es salaam leo  kwa njia ya simu kutokea Dodoma mulugo alisema kuwa maelezo hayo yalitokana na kuchanganya jina la Zimbabwe na Zanzibar” kwanza niombe msamaha kwa yaliyotekea huko unajua ndugu mtangazaji kuna maneno mengi yamesemwa mara eti  sijui kingereza mara sijui historia ya nchi lakini ukweli ni kwamba nilipoenda kuwasilisha hotuba yangu kuna mjumbe kutoka Zimbabwe alikuwa amemaliza kuongea kama dakika mbili tu sasa wakati mimi nikawa nachanganya Zimbabwe na Zanzibar kwa sababu herufi zake zinaanzia na z “ alisema mulugo.

Alipotakiwa kueleza juu ya kukosea mwaka wa kuzaliwa Tanzania  naibu waziri huyo alisema kuwa hiyo inatokana na kuteleza kwa ulimi kwani historia ya cchi hata mtoto wa darasa la pili anaijua” kuna kitu kina itwa lang sleep  wakati nataja mwaka nilikosea nikaongeza namba badala ya kutaja moja nikataja moja moja mbili, mimi nimesoma historia  na uchumi na niliwahi kuwa mwalimu nimefundisha wanafunzi wengi sana  huwezi kusema hata mwaka wa kuzaliwa Tanzania siujui wakati hata mtoto wa darasa la pili anaujua” aliongeza mulugo

Dhahama hiyo imemkumba naibu waziri huyo  wakati akiwasilisha mada yake katika mkutano wa viongozi wa Afrika na taaluma ya elimu uliofanyika nchini  Aafrika ya kusini, Naibu huyo aliwambia wajumbe hao kuwa Tanzania ilizaliwa mwaka 11964 kutokana na muunganiko  wa visiwa  viwili pemba na Zimbabwe, kitu kilichoibua maswali mengi miongozi mwa watanzania juu ya uelewa wa naibu huyo na elimu yake kwa ujumla.

Monday, October 22, 2012

                                                               TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   


            Mpambano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa ngumi nchini Tanzania na Ujerumani kati ya Francis Cheka na Benjamin Simon wa Ujerumani sasa utafanyika tarehe 18 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani.
Awali mpambano huo ulikuwa ufanyike tarehe 17 Novemba mwaka huu jijini Berlin, Ujerumani na tayari bondia Francis Cheka ameshasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la “Iron Ben” kwa ajili ya ukali wa makonde yanayowasulubu wapinzania wake.
Bondia Benjamin Simon ana rekodi ya mapambano 24 ambapo amepoteza pambano moja wakati bondia Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza mapambano 6.
Akimwandikia “Eva Rolle” wa kampuni ya “Primetime Event Management” ya Ujerumani ambaye ndiye promota wa mpambano huo, mwenyekiti wa ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye mwenyewe Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa watakaosimamia mpambano huo.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa wababe hao kukutana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa.
Mshindi katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.
Imetumwa na:
Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais IBF Africa, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi
(IBF Africa, Middle East, Arabian Gulf and Persian Gulf)