Siku chache mara baada ya Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo kudaiwa kubolonga alipokuwa akiwasilisha hotuba yake katika mkutano wa kimataifa kwa kuonyesha mbele ya jamii ya kimataifa kuwa haijui historia ya nchi yake naibu huyo amewaomba radhi watanzania.
Akizungumza katika kipindi cha power break fast kinachorushwa na kituo cha redio clous cha jijini Dar es salaam leo kwa njia ya simu kutokea Dodoma mulugo alisema kuwa maelezo hayo yalitokana na kuchanganya jina la Zimbabwe na Zanzibar” kwanza niombe msamaha kwa yaliyotekea huko unajua ndugu mtangazaji kuna maneno mengi yamesemwa mara eti sijui kingereza mara sijui historia ya nchi lakini ukweli ni kwamba nilipoenda kuwasilisha hotuba yangu kuna mjumbe kutoka Zimbabwe alikuwa amemaliza kuongea kama dakika mbili tu sasa wakati mimi nikawa nachanganya Zimbabwe na Zanzibar kwa sababu herufi zake zinaanzia na z “ alisema mulugo.
Alipotakiwa kueleza juu ya kukosea mwaka wa kuzaliwa Tanzania naibu waziri huyo alisema kuwa hiyo inatokana na kuteleza kwa ulimi kwani historia ya cchi hata mtoto wa darasa la pili anaijua” kuna kitu kina itwa lang sleep wakati nataja mwaka nilikosea nikaongeza namba badala ya kutaja moja nikataja moja moja mbili, mimi nimesoma historia na uchumi na niliwahi kuwa mwalimu nimefundisha wanafunzi wengi sana huwezi kusema hata mwaka wa kuzaliwa Tanzania siujui wakati hata mtoto wa darasa la pili anaujua” aliongeza mulugo
Dhahama hiyo imemkumba naibu waziri huyo wakati akiwasilisha mada yake katika mkutano wa viongozi wa Afrika na taaluma ya elimu uliofanyika nchini Aafrika ya kusini, Naibu huyo aliwambia wajumbe hao kuwa Tanzania ilizaliwa mwaka 11964 kutokana na muunganiko wa visiwa viwili pemba na Zimbabwe, kitu kilichoibua maswali mengi miongozi mwa watanzania juu ya uelewa wa naibu huyo na elimu yake kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment