Thursday, October 25, 2012
MWALIMU WA TLC ASEMA HAWAKO TAYARI KUWAONGEZEA WANAFUNZI SIKU ZA KUSOMA
asisitiza wasiokuwa na gazeti tando (blog)ita kula kwao.
>awasifu wanafunzi kwa kuonyesha nidhamu kwa kipindi chote cha mafunzo..
Mara baada ya uvumi uliokuwa ukisambazwa na baadhi ya wanafunzi, wanaopata mafunzo kwa vitendo katika kituo cha mafunzo kwa vitendo( TLC). Uvumi huo umepingwa vikali na mmoja wa viongozi wa kituo hicho kwa kubainisha kuwa hawafikirii, na hawana mawazo ya kuongeza muda kwa madai kuwa wao wanafanya kazi kwa kufata ratiba ya utendaji kazi wa kituo hicho.
Akizungumza na mwandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es salaam, meneja biashara wa kituo hicho Bw. Dastan Kamanzi alisema kuwa uvumi huo hauna chembe hata moja ya ukweli, kwa kuwa wao wanafanya kazi kwa kufuata ratiba ya kituo hicho” swala hilo la kuongeza muda halina ukweli wowote kwa sababu tunafata ratiba na tunakazi nyingi za kufanya pia muda uliokuwa umepangwa umekwisha na tutakuwa na kazi ya kuandaa matokeo ya wanafunzi “alisema kamanzi.na kuongeza kuwa wao hawana lengo la kumfelisha mtu bali haki itatendeka kwa kila kazi iliyofanywa na mwanafunzi.
Akizidi kufafanua kwa undani zaidi jinsi mafunzo yalivyoendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu, kamanzi alisema kuwa wamefundisha kila kitu ambacho walitakiwa kukifundisha hivyo hakuna mada iliyoachwa kwani wao wanafundisha kwa kufuata mtaala, “kila mwalimu amefundisha mada zote kama inavyotakiwa. Akitolea mfano kwenye somo la new media kila mwanafunzi kafundishwa jinsi ya kufungua blog, sasa kuna haja gani ya kuongeza muda wakati kila kitu kimefundishwa” alisema kamanzi, pia alikemea tabia ya wanafunzi wanaofungua blog kwa lengo la kupata alama pasipo kujua kuwa zina faida kubwa kwao kama wakiziendeleza“ kuna wanafunzi wakisha sahihishiwa na kupewa alama zile blog zao wanaziacha hivyo si vizuri kwani blog wakiziendeleza wanaweza kujipatia kipato kwa kuweka matangazo ya watu mbalimbali lakini wao hawalijui hilo” aliongeza kamanzi.
Akiendelea kutoa ufafanuzi kwa undani zaidi na jinsi wanavyopata changamoto walizokutana nazo Bw. Kamanzi alisema kuwa darasa la awamu hii halikuwa na matatizo, kama ya awamu iliyopita kutokana na wanafunzi kuwa na nidhamu ya hari ya juu. Na kutolea mfano suala la wizi na kugombana matatizo ambayo yalijitokeza katika awamu iliyopita, pia alitoa wito kwa wanafunzi wasio kuwa na brog kuwa nazo kwani kutokuwa nazo kutawapunguzia alama na kuwataka wanafunzi ambao hawajamaliza kazi zao kukamilisha na kuzipeleka kwa walimu husika.
Nae mwanafunzi wa kituo hicho Exuad Mtei alisema kuwa uvumi huo haukumuathili kitu chochote kitaaluma kwa kuwa hadaiwi kazi yoyote na mwalimu” mimi waongeze muda wasiongeze sina shida kazi kwao ambao kawajamaliza kazi za walimu wao. Pia naunga mkono kauli ya kutoongeza mda kwa sababu hata mimi nina shughuli zangu za msingi nahitaji kuzifanya wakiongeza muda wataniharibia ratiba” alisema Bw. Mtei, huku baadhi ya wanafunzi wakikataa kulizumngumzia suala hilo.
Kituo cha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari TIME (TSJ) kilianzishwa mnamo mwaka 2010, chini ya udhamini wa mwaka mmoja kutoka Tanzania Media Fund ( TMF).Nia na Madhumuni na lengo la kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo. Katika Nyanja mbalimbali za Utangazaji,kama vile Radio, Television production, Printing na photo journalism kwa wanafunzi wa Stashada ya nne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment