Msanii Country Boy akipagawisha mashabiki kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe kama Lote Mkoani Mwanza |
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota mkoa wa Mwanza 2018, Elisayo akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana uwanja wa CCM Kirumba |
Msanii anayechipukia, Jollie akiwa kwenye steji ya Tigo Fiesta Vibe Kama Lote usiku wa kuamkia jana uwanja wa CCM Kirumba
|
Kundi la Weusi lilkipagawasha mashabiki kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza usiku wa kuamkia jana |
Wakaazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake usiku wa
kuamkia jana waliweza kukonga mioyo yao kwa burudani kabambe kwenye Tamasha
kubwa nchini la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba.
Wasanii mbalimbali wakiwemo Weusi, Rostam, Country Boy,
Nandy, Fid Q, Richie Mavoko, Jux,WhoZu Nedy Music na wengine wengi waliweza
kufanya kile mashabiki walikuwa wanatarajia.
Mwamba wa kanda ya Ziwa Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q
aliwateka vilivyo wanamwanza hasa kwa wimbo wake FRESH, Fid Q ambaye ni
mwenyeji wa Mwanza ilimbidi arudie wimbo huo pendwa mbele ya mashabiki.
Vibe la Tigo Fiesta liliamshwa zaidi na kundi la Weusi
lililowajumuisha Joh Makini, Nikki wa Pili , Lord Eyez na G Nako walioweza kukaa
jukwaani kwa muda mrefu bila kuchosha mashabiki kwa nyimbo lukuki zikiwemo
SWAGIRE,NiCome na kadhalika.
Nae Msanii anayeng’ara kwa sasa, WhoZu aliweza kuwakamata
mashabiki kwa wimbo wake HUENDI MBINGUNI amabo ameupiga kwa mahadhi ya Reggae.
Kwa upande wa kundi la Rostam linalowajumuisha Roma na Stamina kama kawaida yao
wao ndio wanaofunga jukwaa, waliweza kufunga shoo kwa nyimbo zao nyingi.
Nao Wadhamini wa Tamasha hilo Kampuni ya Tigo, Mkurugenzi wa
Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madata alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia
wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti
watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa
mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta
2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa
4G+,’ Madata alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10
millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za
TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo.
Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571
au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz
Tamasha hilo litaendelea jumapili hii kwenye uwanja wa Karume
mjini Musoma.
No comments:
Post a Comment