Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano wa makabidhiano.
|
Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada
wenye thamani ya milioni 6 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya
Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa hafla
ya makabidhiano Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa
benki hiyo, Christine Manyenye alisema kuwa mchango huo upo ndani ya
vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia
jamii zilizo na uhitaji.
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini
uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya
vipaumbele vya Afya, Elimu, Mazingira, Ujasiriamali na masuala ya ubinadamu”,
Bi. Manyenye alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofungua milango
yake hapa Tanzania mwaka 1997, imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.
Benki ya KCB ilikabidhi
misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani
ya shilling 6,017,000 katika Hospitali hiyo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa upungufu
wa vitanda, magodoro na masuka katika hospitali nyingi nchini ni changamoto hasa
katika wodi za akina mama na watoto Benki ya KCB iliamua kutoa msaada huo
ilikupunguza changamoto hizo.
Akitolea mfano wa michango
iliyotolewa na benki hiyo katika kupunguza viwango vya vifo vya kinamama
na watoto nchini, Manyenye alisema: “Kupitia miradi hiyo Benki ya KCB Tanzania
imeshazisaidia hospitali zaidi ya 15 kwa kuzipatia vifaa tiba mbalimbali.”
Alizitaja hospitali hizo kuwa
ni Muhimbili, Mwananyamala, Ocean Road Cancer Institute, Buguruni, Sinza,
Amana, Temeke na Kituo cha Afya cha Njia (Dar es Salaam); Mt. Meru
na Ngarenaro (Arusha); KCMC, St. Thomas na Mawenzi (Moshi); SDA na Makongoro
(Mwanza); Hospitali ya Morogoro (Morogoro); Kivunge Cottage na Kituo
cha Huduma za Afya Kombeni (Zanzibar) na Hospitali
ya Mkuranga (Pwani).
Kwa upande wake, Kaimu Mganga
Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dr. Amim Kilomoni aliishukuru KCB Bank kwa msaada
waliotoa kwani utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili, ikiwamo
uhaba wa vitanda, magodoro na mashuka.
No comments:
Post a Comment