Mwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama na kulia ni mwimbaji Bonny Mwaitege. (Picha na Habari Mseto Blog)Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kuwatambulisha wanamuziki wataoshiriki tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama.Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatambulisha baadhi ya waimbaji watakaoshirika katika tamasha la Pasaka 2013. WAIMBAJI Upendo Nkone na Boniface Mwaitege wamesema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufikisha neno la mungu kwa waamini watakaojitokeza siku ya tamasha hilo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na waandishi wa habari, Nkone alisema inaonekana ana wapenzi wengi zaidi katika nyimbo za kumtukuza mungu ndio maana wamemchagua kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi, hivyo ana deni la kuwalipa siku hiyo.
“Nimepata furaha kwa waamini kutambua kazi yangu, ndio maana na mimni najihisi nna deni, na nawaahidi kuimba wimbo mpya siku hiyo ambao “Nimebaki na Yesu” ambao unachochea ibada kwa waamini,” alisema Nkone.
Nkone alisema uimbaji wa nyimbo za injili ni mgumu iwapo utafanya vibaya na jamii pia itakukataa ambako pia waamini wanatakliwa kuisoma biblia na kuielewa sambamba na kumuomba mungu kwa dhati ya kweli.
Naye Mwaitege alisema amefurahi kupata bahati ya kuwa mmoja wa wahudumu wa neno la mungu siku hiyo kwa sababu tamasha la mwaka jana hakupata bahati ya kushiriki kwa sababu alikuwa safarini nchini Kenya.
“Mwaka jana nilitamani kuimba pamoja na Rebecca Malope lakini bahati haikuwa yangu, ingawa nimepata bahati ya kuimba na Sipho Mwakabane ambaye naye anatokea Afrika Kusini kama Malope na Watanzania wenzangu kama akina John Lissu, Upendo Kilahiro na Rose Muhando,” alisema Mwaitege.
Aidha Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema siku ya Tamasha utafanyika uzinduzi wa albam ya kundi la Gloria Celebrations ‘Kwetu Pazuri’ itakayojulikana kama ‘Kuweni Macho’ ambayo itauzwa siku hiyo.
Tamasha hilo ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Mbeya Aprili Mosi, Iringa Aprili 3, Aprili 6 mkoani Dodoma na Mwanza Aprili 7.
Viingilio katika tamasha hilo kwa VIP ni shilingi 50,000, Viti maalum shilingi 10,000, Viti vya kawaida 5000 na watoto shilingi 2000.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda