Fanya
malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama zaidi kwa zaidi ya idara 300 za serikali,
mawakala na mamlaka za udhibiti kwa Tigo Pesa
Wateja
wa Kampuni ya Tigo, sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki
wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini
kwenye App yake ya Tigo Pesa.
Akiongea katika uzinduzi wa GePG kwa
mtandao wa Tigo yaliyofanyika jijini Dar
es Salaam, Bernard Mabagala Afisa Mwandamizi wa TEHAMA – Wizara ya Fedha na
Mipango alisema kuwa ubunifu na juhudi za Serikali katika kuanzisha mdumo huo wa Kieletronbiki wa
Malipo Serikalini (GePG) umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo
kwa wananchi. Pia imeleta faida nyinginezo ikiwemo kuboresha uwekaji wa
kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvuvaji na ubadhirifu pamoja na
kuongeza mapato kwa idara mbali mbali za Serikali. na
Kupitia mfumo wa GePG Serikali pia
imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za
biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza
kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali au kwa
njia mbali mbali za kimtandao, na kufanya malipo ya ankara kwa urahisi na
mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.
“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali
ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo na mkakati
wetu,” alisema Hussein Sayed, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kifedha wa Tigo.
“Zaidi ya wateja milioni 7
wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa
haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia
Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Biashara
na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya.
Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo
Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Shirika la Kodi Tanzania (TRA), Shirika la
Umeme Tanzania TANESCO, Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
Shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi,
Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara Malia Asili na Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya
Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA),
Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile
Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300.
Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo
wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya
siri ili kufanikisha muamala.
Ili kufanya malipo kwa kutumia menu ya Tigo Pesa, mteja anatakiwa kufuata
hatua zifuatazo;.
1)
Kupiga *150*01# kisha kuchagua Lipa Bili
2)
Kuchagua namba 5 (Malipo ya Serikali)
3)
Kuingiza tarakimu 12 za mamlaka au taasisi anayotaka
ipokee malipo
4)
Kuingiza kiasi cha fedha anachotaka kulipa
5)
Kuingiza namba ya siri kwa ajili ya kuruhusu malipo
Kwa upande mwingine, wateja
wanaweza kutumia App ya Tigo Pesa ambayo inarahisisha ufanyaji wa malipo kwa kiasi
kikubwa.
Baada ya kukamilisha malipo, wateja
wa Tigo watapokea risiti ya kielektoniki kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi
unaothibitisha kuwa muamala umefanyika kikamilifu. Risiti hiyo ya kielektroniki
inakubalika kama uthibitisho tosha wa malipo na inaweza kusaidia kurahisisha
kufuatilia malipo kwa kuwa ni rahisi kuhifadhi na kuipata pale inapohitajika
ukilinganisha na risiti za karatasi ambazo ni rahisi kupotea au kuharibika.
Tigo inawakaribisha
wateja wake kuanza kutumia huduma hii ya Malipo ya Kieletroniki Serikalini
(GepG) sasa.
No comments:
Post a Comment