|
|
Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki Rich
Mavoko, akiwaburudisha mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na maeneo
jirani walioshiriki katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika
katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani humo.
|
Msanii wa Bongo Flava ambaye ni zao la kundi la Tip Top
Connection la jijini Dar es Salaam Dogo Janja au akitoa burudani
kwa mamia ya mashabiki
walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja
wa Jamuhuri Mkoani Dodoma.
|
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Whozu pamoja na madensa wake wakilimiliki vilivyo jukwaa wakati wa alipokuwa akitoa murudani ya kufunga mwaka kwenye Tigo
Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja wa David Zimbihile Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
|
Msanii Rosalee akifanya yake katika tamasha la Tigo Fiesta
mwaka 2018 lililofanyika uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
|
-Baadhi ya Wabunge wapanda jukwaani kusakata Kwaito, Bolingo
-Bill Nas, Weusi
, Whozu, Rosaree waacha historia
Na MWANDISHI WETU
Wabunge na viongozi wa Serikali, jana walikuwa ni sehemu
ya burudani ya aina yake katika Tamasha
kubwa la muziki la Tigo Fiesta 2018,
lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Tamasha hilo lililofanikiwa kuwavuta mashabiki wa muziki
wa bongo fleva kutoka mkoa huo na viunga vyake, lilianza kwa msanii Jay Melody
kupanda jukwaani na kutoa burudani safi
‘iliyobamba’na kutengeneza mazingira safi
kwa waliomfuatia
Baada ya wasanii kadhaa kupanda jukwaani i, Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi alipanda jukwaani kuongea mawili matatu kabla
ya kuomba kuwekewa muziki wa bolingo ambalo alisakata kwa ustadi kmubwa jambo
lililozua shangwe za ktosha.
Wakati Katambi akiendelea kusakata bolingo, baadhi ya
wabunge wakiongozwa na mbunge wa Sengerema William Ngeleja waliomba kuwekewa muziki wa Kwaito
ambao waliusakata kwa ufundi mkubwa na kusababisha shangwe kubwa kutoka kwa
mashabiki.
Wasanii wanaounda
kundi la Weusi, Bill Nas, Barnaba, Rosaree ni baadhi ambao wataendelea
kukumbukwa na wakazi wa Dodoma kutokana na kutoa burudani safi kwa wakazi hao
ambao walionekana kuwa na kiu ya buruidani
Ili kunogesha msimu wa Tigo
Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za mkononi ya Tigo imewaletea promosheni
bab-kubwa inayojulikana ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa
vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja wa
Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo
4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema katika tamasha
la Mwanza.
Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za
tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
Wateja wanapaswa kupiga *150*01#
na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR)
na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa
kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.
Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi
za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000
kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla.
Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI
kwenda 15571 au kutembelea
tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua
Trivia.
No comments:
Post a Comment