Friday, April 12, 2013

MWIGULU NCHEMBA ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI,MBOWE NA SLAA WAKAMATWE KWA UGAIDI

 

 

mwigulu nchemba bungeni


  • MWIGULU NCHEMBA:- Dr. SLAA NA MBOWE WAKAMATWE KWA UGAIDI!




  • SPIKA ASHANGILIA NA KUSEMA MKUKI KWA NGURUWE  WABUNGE WAMSHANGA.




  • TUNDU LISSU AMSHUSHUA SPIKA KWA KUSEMA SUALA LA MAWASILIANO KUHUSIANA NA KESI YA UGAIDI NA MARAFIKI ZAO HALIPO MAHAKAMANI.




Mwigulu Nchemba ameibuka na kile kilichotarajiwa kwa kuongelea suala la Mkanda wa Lwakatare huku akiwaomba Polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA kwa ugaidi


Akichangia bungeni muda huu Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare jinsi alivyoipata, kiongozi wa CHADEMA aliyempa pia yupo tayari. Amelitaka jeshi la polisi limkamate Mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE.




Awali Mwigulu alisimama na kushambulia CHADEMA na viongozi wake hasa Mbowe kwa kumtaja jina na akisema hawa wote ni magaidi hali iliyopelekea Joseph Selasini aombe utaratibu kumtaka Mwigulu kufuta kauli yake ya kumshambulia Mbowe kibinafsi na kumtaka aache kuongele swala lililo mahakamani. Spika akuchukuwa hatua yoyote lakini pale aliposimama Tundu Lissu na kujibu hoja ya Mwigulu ndipo Spika alipo ibuka na kusema inatakiwa Mahakama ilindwe na kuheshimiwa bila kuingiliwa.


Akijibu hoja ya Spika kwamba masuala yaliyopo mahakamani yaheshimiwe:




“Mheshimiwa Spika, suala la mawasiliano kuhusiana na kesi ya ugaidi na marafiki zao humu ndani halipo mahakamani.”


Source: TBC1 Live coverage



No comments: