Tume ya kulinda amani ya umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, imelaani hatua ya kuzuiliwa kwa malori yake 10 yaliyokuwa yakibeba makontena.
Magari hayo ya Umoja wa mataifa yaaminika kutokea Entebbe nchini Uganda, ambako tume hiyo imekuwa pia na ngome yake. Magari hayo yamezuiliwa na waasi wa kundi la M23 mtaani Rutshuru, huku waasi hao wakilazimisha kufunguliwa kwa makontena hayo ili wachunguze vitu vilivyowekwa ndani. Msemaji wa MONUSCO, Madnodje Munubai, ameitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa kanuni za kimataifa. Hadi sasa magari hayo yanaendelea kuzuiliwa na waasi wa M23. Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo anaarifu kutoka Kinshasa. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Josephat Charo
No comments:
Post a Comment