Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE amewapandisha vyeo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi kuwa makamishna wa polisi(CP) na manaibu kamishna wa polisi (DCP)
Katika taarifa iliyotolewa leo ikulu jijini dar es salaam imewataja waliopandishwa kuwa makamishna ni ISAYA MUNGULU na SULEMAN KOVA ambao kabla ya vyeo vyao vipya walikuwa manaibu kamishna wa pilisi
Aidha waliopandishwa kuwa manaibu kamishna wa polisi ni ELICE MAPUNDA,BROWN LEKEY,HAMDAN OMAR MAKAME,KENETH KASSEKE,ABDUL RAHMAN KANIK,THOBIAS ANDENGENYE,ADRIAN MAGAYANGE,SOSPETER KONDELA,SIMON SIRO NA ERNEST MANGU.ambapo kabla ya uteuzi huo maafisa hao walikuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa polisi
Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja
No comments:
Post a Comment