Kombe la FA likiwasilishwa uwanjani
Joe Hart akiruka bila mafanikio
Makocha wa Man city na Wigan wakati wote wa mchezo walikuwa na hekaheka
Ben Watson akishangilia bao lake la ubingwa wa FA
BAO la Ben Watson katika dakika ya mwisho kabisa jioni hii limeipa Wigan ubingwa wa Kombe la FA kwa mara ya kwanza kabisa ikiichapa Manchester City 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley.
Nyota huyo aliyetokea benchi alifunga kwa kichwa akiunganisha kona na kuwa shujaa wa mashabiki wa Wigan na kumfanya Roberto Mancini arejee nyumbani mikono mitupu.
Man City ilimaliza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekundu daika ya 84.
Katika mchezo huo, kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Silva, Toure , Barry/Dzeko dk90, Nasri/Milner dk54, Aguero na Tevez/Rodwell dk69.
Wigan: Robles, Boyce, Scharner, Alcaraz, Espinoza, McCarthy, McArthur, Gomez/Watson dk81, McManaman, Kone na Maloney. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment