WATANZANIA wanaoishi nchini Afrika Kusini na nchi jirani ya
Botswana leo wamejitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea,jumanne mwili
wa marehemu unatarajia kuwasili nchini Tanzania na kupelekwa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa, kabla ya shuguli za kuuaga tena kufanyika
katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mangwea aliagwa na umati wa watu mbalimbali wakiwemo
Watanzania na watu wa mataifa mbalimbali wanaoishi nchini Afrika Kusini, jijini
Dar es Salaam pia kutakuwa na zoezi kama hilo siku ya Jumanne kabla ya
kusafirishwa hadi mjini Morogoro kwa mazishi siku ya Jumatano
Pamoja na kwamba Mangwea anatarajia kuzikwa mjini
Morogoro, utata juu ya ripoti ya uchunguzi wa kifo chake imeanza kutawala,
baada ya kuwepo kwa mvutano wa kuifanya ripoti hiyo kuwa siri, huku baadhi ya
watu wakitaka ripoti itangazwe kama ilivyoandikwa na jopo la Madaktari
wa Hospitali ya St Hellena Joseph.
Inaelezwa kwamba
familia ya msanii huyo imekataa kuweka wazi sababu za kifo cha mtoto wao,
"Ripoti ya Uchunguzi wa Madaktari imetoka lakini haturuhusiwi kuitoa kwa
sababu ndugu zake wamekataa, ila kuiona nimeiona na siwezi kukwambia kwamba
inasemaje"alisema mmoja wa watu wa karibu wanaoshugulikia taratibu za
kusafirisha mwili wa marehemu kuja nchini Tanzania katika mahojiano maalumu na Habari24
Habari24 pia ilijaribu kuwasiliana na ndugu na
jamaa wa Ngwea nchini Tanzania na kudai kwamba, ni kweli ripoti ya uchunguzo wa
Madaktai umetoka lakini wao kama familia hawajaiona. "Nikweli tumesikia hivyo, lakini
hatujui chochote kilichoandikwa na Madaktari, hivyo hatuwezi kuizungumzia,
ingawa mimi pia siyo msemaji wa familia, lakini hata ukiwaona wahusika bado
hawatakuwa na majibu yoyote kwa sababu wao wako Tanzania na ripoti bado iko
Afrika Kusini"alisema mmoja wa wanafamilia wa marehemu ambaye hakutaja jina
lake liandikwe ndani ya mtandao wa Habari24
No comments:
Post a Comment