MAMIA YA MADEREVA WALIOJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MKUTANO HUO ULIOMALIZIKA MUDA HUU HAPA DAR LIVE DAR ES SALAAM |
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MADEREVA WA MALORI YAENDAYO TANZANIA ( CHAMAMATA) BW CLEMENT MASANJA AKISISITIZA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO |
Akizungumza
katika mkutano wa dharura uliowakutanisha madereva wote wa malori nchini na
wanachama wote wa chama hicho kwa lengo la kujadili maslahi yao mwenyekiti wa UMAMATA
bw CLEMENT
MASANJA amesema madereva sasa wamechoshwa na hali hiyo ya
kufanya kazi bila mikataba na wameona ni bora kutoa sauti zao kwa serikali
Bw MASANJA
amesema kuwa kutokuwepo kwa mikataba ya kudumu kwa madereva hao kutoka kwa
mabosi wao kimesababisha kutokuelewa haki zao kama waajiriwa jambo
linalowavunja moyo katika kazi zao
Aidha amesema
umefika wakati sasa wa polisi wa usalama barabarani kuanza msako maalumu wa
kukagua mikataba ya madereva kama wanavyokagua leseni za udereva na kama
watabaini kuna dereva anafanya kazi bila mkataba basi hatua kali ichukuliwe juu
ya kampuni husika
Katika
hatua nyingine madereva hao kwa umoja wao wameadhimia kukutana na waziri wa
uchukuzi dk HARISON MWAKYEMBE
pamoja na SUMATRA kwa lengo la kueleza jinsi
wanavyonyanyaswa na waajiri wao ikiwemo maslahi duni wanayoyapata.
VIONGOZI WA CHAMAMATA WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO |
1 comment:
sawa
Post a Comment