Wednesday, June 26, 2013

MAZOEZI SIMBA SC YAZIDI KUCHANGANYA...HANS POPPE AJIONEA MWENYEWE STRAIKA KUTOKA CAMEROON

HABARI KWA HISANI YA BIN ZUBEIR BLOG
IMEWEKWA JUNI 26, 2013 SAA 1:05 USIKU

Kifaa kutoka Cameroon; Mshambuliaji raia wa DRC, Felix Cuipoi akimtoka beki William Lucian 'Gallas' katika mazoezi ya Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam. Cuipoi amesema amekuja kufanya majaribio Msimbazi, akitokea klabu ya Eagles FC ya Cameroon na msimu uliopita alishika nafasi ya tatu kwa ufungaji wa mabao, akifunga mara 19.
Cuipoi nna Gallas
Patashika ile hadi kivumbi mazoezi ya Simba SC Kinesi leo
Mshambuliaji mpya Zahor Pazi akipasua
Mazoezi ya nguvu, kushoto Nahodha mpya, Nassor Masoud 'Chollo'
Mazoezi ya minyumbuliko
Tiba; Daktari mpya wa Simba SC, Yassin Gembe akimchua misuli kiungo mshambuliaji, Haruna Chanongo
Kocha wa Simba SC, Abdallah Kibadeni kulia akiwa na kiungo Amri Kiemba
Wanazungumza
Simba TV; Zahor Pazi akiigiza mtangazaji wa TV kwa kumuhoji mchezaji mwenzake, Haruna Shamte kulia
Gari Kubwa; Nahodha wa zamani wa Simba SC, Willy Martine 'Gari Kubwa' (katikati) alikuwepo mazoezini leo Kinesi 
Gwiji; Mchezaji na kiongozi wa zamani wa Simba SC, tangu enzi za Sunderland, Hamisi Kilomoni akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Said Pamba kulia Kinesi leo
Bosi kubwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akiwasili mazoezini

Anamsalimia Mzee Kilomoni
Anasalimiana na Geoffrey Nyange 'Kaburu' kulia. Katikati ni Katibu, Evodius Mtawala.
Asije kuwa Jama Mba mwingine huyu!; Anaangalia mazoezi kwa makini kabisa

No comments: