Monday, June 3, 2013

RASIMU YA KATIBA YAZINDULIWA ZITO KABWE ATOA YA MOYONI KUHUSU UMRI WA MGOMBEA URAISI

MH ZITO KABWE AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI NJE YA UKUMBI BAADA YA KUZINDULIWA RASMI RASIMU YA  KATIBA MPYA
 Mwenyekiti wa tume ya katiba mpya jaji warioba amesema Rasimu inapendekeza miaka 40 ya Mgombea Urais.Miaka 40 ndipo mtu atakuwa na sifa ya kugombea urais.
Baad aya kupata habari hizio,nje ya ukumbi ambapo uzinduzi wa rasimu unafanyika habari 24 inakutana na zito kabwe na kumuuliza anasemaje kuhusu Umri huo uliotangazwa.kwanini tumemtafuta zitto kabwe?Tumemtafuta Zitto Kabwe kwa sababu ni moja ya vijana wanasiasa machachari sana na yupo midomoni mwa watu sana Kuelekea uchaguzi wa Mwaka 2015 ambapo amekuwa akitajwa kuwania Urais.
Na katika moja ya mahojiano yake siku za nyuma na vyombo vya habari alikili wazi yeye anataka kugombea Urais mwaka 2015 endapo chama chake kitamruhusu.
Baada ya kutafutwa aelezea alivypokea miaka 40 ya mgombea Urais alikuwa na hiki cha kujibu
"
Rasimu imeshaeleza hilo kuwa wanapendekeza miaka 40,Kwanza sipendi kabisa kuongelea swala la urais kama nilivyoahidi kwa mwaka 2013.Lakini nasisitiza Miaka 10 jimboni inatosha sana. Sitagombea Kgm kaskazini tena.Huu ndio msimamo wangu".


No comments: