Monday, July 1, 2013

AJIRA KWA VIJANA ZAONGEZEKA



 
 Serikari ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeongeza ajira kwa  vijana kwa kujenga viwanda vikubwa hapa nchini ambavyo vitaweza kuiendeleza nchi katika swala zima la ukuaji wa kipato.

      Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam waziri wa Nishati na Madini Proffesa SOSPETER MUHONGO amesema kuwa serikali imeona vyema kusajili viwanda ili kuongeza ajira kwa vijana na katika kuona hilo wameona wasajili kiwanda cha saruji DANGOTE kilichopo mtwara ili kiweze kuongeza uchumi wa nchi.

       Proffesa MUHONGO ameongezea kwa kusema kiwanda hiki kimepata leseni ya uchimbaji katika kutengeneza saruji na pia kutokana na kuwa na uzoefu katika kufungua viwanda katika nchi  takriban 20 wawekezaji hawa wa DANGOTE watazalisha umeme wao Mega watts 70 kwa kutumia gesi,umeme utakao baki utakuwa wa Taifa.

           Kiwanda cha saruji DANGOTE kime wekeza dollar za kimarekani Million 5 katika awamu ya kwanza ya kuendesha kazi na pia kinategemea katika awamu hii ya kwanza wazalishe tani Million 300

No comments: