Monday, July 1, 2013

SERIKALI IWAJALI WAFANYAKAZI WAKE---TUCTA



 

 Serikali imetakiwa kuwajali wafanyakazi wake ikiwemo kuyapa kipaumbele madai yote ya wafanyakazi hao jambo ambalo limetajwa kuondoa manunguniko ya wafanya kazi juu ya serikali yao
           Akizungumza na upendo radio katibu mkuu wa shirikisho la wafanyakazi tanzania TUCTA bw NICOLAUS MGAYA amesema kuwa madai ya wafanyakazi yapo kila mwaka linalotakiwa kufanywa na serikali ni kuhakikisha linayapa kipaumbele ili kuwapa imani wafanyakazi juu ya serikali yao
        Bw MGAYA amesema kuwa serikali yoyote duniani uchumi wake unakuwa kutokana na kazi za wafanyakazi wake hivyo ni lazima serikali iwajali wafanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kuwalipa kwa wakati ili kuepuka wafanyakazi kufanya kazi bila matumaini na serikali yao.
         
 Akizungumzia madai ya malimbikizo ya malipo ya walimu ambao hivi mapema walitangaza kuwa wapo katika mpango wa kuandaa maandamano ya kudai malimbikizo hayo  bw MGAYA amewataka waalimu kuwa na subira kwani bado mazungumzo na serikali yaaendelea huku akisema mh RAISI amewaahidi kukutana nao mapema mwezi huu ili kujadili madai hayo
       
     Amesema kwa kuwa raisi wa tanzania amekuwa msikivu kwa wafanya kazi na kukubali kukutana nao ni lazima kwa walimu kuvuta subira kwanza hadi mazungumzo hayo yafanyike kwani moja ya ajenda kubwa ya kikao hicho ni madai ya walimu.

No comments: