Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe,Meck Sadick alipokuwa akizungumza
katika kipindi kilichokuwa kikionyeshwa Live na Televishion ya Taifa
(TBC ) alisema kuwa wote wanaopanga kuandamana leo kwanza haitaruhisiwa
na pia kuandamana ni Ushamba aliyasema hayo pale alipo ulizwa swali na
Mtangazaji aliekuwa anamfanyia mahojiano kuhusu Maandalizi ya kumpokea
Rais wa Marekani Barrac Obama na njia ambazo atapitia rais huyo kipindi
atakacho kuwepo nchini kwa siku mbili.Swali lilikuwa hivi Mheshimiwa
Mkuu wa mkoa je unataarifa zozote au kama kuna maombi ambayo yamekufikia
kwamba kuna watu ama vikundi vinavyotaka kuandamana kama walivyofanya
Waandamanaji Afrika kusini majibu ya mkuu huyo wa mkoa yalikuwa "Kwanza
niseme tu Kuandamana ni Ushamba na kwa nini mtu aandamane wakati wa
ziara ya Rais Obama" akaendelea kwa kusema "Maandamano yeyote yale
kimsingi huwa ayana maana yeyote ile kwa sababu hata ukiandamana
haitakusaidia zaidi ya kukupotezea mda sisi tunatoa wito kama kuna watu
wenye nia hiyo tunawaomba waache na wajitokeze tu kumpokea mgeni kwa
Amani lakini tukiona kunaviashilia vyovyote vya maandamano
tutawakamata".Rais Obama anatarajiwa kufika majira ya saa 8:40 mchana na
Barabara atakazopitia wakati akitoka uwanja wa Ndege zinatarajiwa
kufungwa kuanzia saa 6:30 mchana.
|
No comments:
Post a Comment