BAADH YA WAWAKILISHI WA MAKAMPUNI HAYO YA SIMU NA BENKI WAKIWA KATIKA UZINDUZI HUO |
BW JACKSON MIDALA MABAYE NI AFISA MTENDAJI MKUU WA DAWASCO AKIONYESHA BAADH YA MASHINE ZITAKAZOTUMIKA KATIKA KULIPIA BILI |
Shirika la maji safi na maji taka dar es salaam DAWASCO limezindua rasmi mpango wake kwa wateja kulipa malipo ya huduma ya maji kwa kutumia technologia jambo ambalo litasaidia kurahisisha huduma hiyo kwa wateja wake
Akizumgumza katika uzinduzi huo afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO bwJACKSONI MIDALA amesema kuwa njia hiyo itawafanya wateja wengi kuweza kulipia bili ya maji kwa urahisi na haraka zaidi tofauti na ilipokuwa hapo awali ambapo wateja walilazimika kufika katika ofisi zao kwa ajili ya malipo
Katika huduma hiyo wateja wa maji dar es salaam wataweza kulipa bili zao kwa kutumia mitandao yote ya simu Tanzania pamoja na baaadhi ya benki hapa nchini ambapo mfumo huo umeelezwa kusaidia kupunguza msongamano uliokuwepo katika maofisi ya dawasco wakati wa kulipa bili
Aidha Bw MIDALA amesema kuwa wapo wateja na wananchi waopotoshwa kuwa huduma hiyo sio salama ambao amewatoa wasiwasi na kusema kuwa huduma hiyo ni salama na ni njia nzuri zaidi kulilo iliyokuwa inatumika hapo awali.
WAANDISHI WA HABARI WALIOHUDHURIA WAKISIKILIZA KWA MAKINI |
No comments:
Post a Comment