Thursday, August 1, 2013

EXCLUSIVE ----MTOTO WA MIAKA 14 YATIMA MTANZANIA AISHANGAZA DUNIA,AONYESHA KIPAJI CHA AJABU

MTOTO HANIS MOHAMED KONDO BINGWA WA MASHINDANO YA KURUKA KAMBA DUNIANI AMBAYE NI MTANZANIA AKIONYESHA KIKOMBE CHAKE ALICHOKICHUKUA HUKO MAREKANI 


HAPA AKIMKABIDHI MWAKILISHI WA SERIKALI KIKOMBE HICHO ISHARA YA KUISHUKURU SERIKALI KWA SAPOT YAO


HAWA NI BAADHI YA WATANZANIA WENGINE AMBAO NAO WALISHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO

         MTOTO AMBAYE NI YATIMA KUTOKA TANZANIA MWENYE UMRI WA MIAKA 14 AMEISHANGAZA DUNIA KWA KUIBUKA BINGWA NAMBA MOJA KATIKA MASHINDANO YA KURUKA KAMBA YALIYOFANYIKA NCHINI MAREKANI NA KUSHIRIKISHA WASHIRIKI ZAIDI YA 400 KUTOKA KILA POANDE YA DUNIA 

            MTOTO HUYO AMBAYE NI HAMISI KONDO AMEILETEA SIFA KUBWA TANZANIA KWA KUWA BINGWA WA MCHEZO HUO AMBAO SASA UNAANZA KUJICHUKULIA UMAARUFU MKUBWA KATIKA NCHI ZA ULAYA NA AFRICA KWA UJUMLA,

            AKIZUNGUMZA BAADA YA KUWASILI TANZANIA AKIWA NA KOMBE LAKE MTOTO HUYO AMBAYE NI YATIMA KUTOKA KITUO CHA DOGO DOGO CENTER NCHINI TANZANIA AMEONYESHA FURAHA YAKE KWA KUFANUKIWA KUFIKIA HATUA HIYO NA KUAHIDI KUENDELEA KUIWAKILISHA VYEMA TANZANIA KATIKA MICHUANO HIYO

             MTOTO HUYO AMEKUWA KIVUTIO KIKUBWA SANA LEO KWA WANAHABARI LEO KUTOKANA NA UWEZO WAKE WA KURUKA KAMBA KWA STAILI MBALIMBALI AMBAZO ZINAONYESHA WAZI KUWA YEYE SIO BINGWA WA KUBAHATISHA KAMA UNAVYOPATA KIONJO KATIKA PICHA HAPO

PICHA MBILI HIZI NI HAMIS KONDO AKIONYESHA MAMBO YAKE MBELE YA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM



WAANDISHI WA HABARI NA WADAU WA MCHEZO HUO WA KURUKA KAMBA NAO WALIKUWEPO KATIKATI NI BLOGER KUTOKA BLOG MOJA WAPO HAPA MJINI AKISIKILIZA KWA MAKINI 


No comments: