Thursday, August 1, 2013

exclusive -- KESI DHIDI YA WAZIRI MKUU PINDA YATINGA MAHAKAMANI LEO



      


      KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU LHRC KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA TANGANYIKA LAW SOCIETY LEO WAMEFANYA KILE WALICHOKITANGAZA JUZI KWA KUFUNGUA KESI KATIKA MAHAKAMA KUU JUU YA WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH MIZENGO KAYANZA PINDA KUTOKANA NA KAULI ZAKE ALIZOZITOA KATIKA BUNGE LILILOPITA

       KATIKA KESI HIYO ILIYOFUNGULIWA MAHAKAMA KUU NA KITUO HICHO INADAI KUWA WAZIRI MKUU PINDA ALITOA MANENO YA KUWASHAWISHI POLISI NA VYOMBO VYA USALAMA KUWAPIGA WANANCHI PINDI WATAKAPOLETA FUJO KITU AMBACHO NI KINYUME NA KATIBA YA TANZANIA AMBAYO INAMTAKA ASKARI KUMKAMATA MHALIFU NA KUMFIKISHA KATIKA VYOMBO HUSIKA IKIWEMO MAHAKAMANI

AKIZUNGUMZA BAADA YA KUFUNGUA KESI HIYO MKURUGENZI MKUU WA LHRC BI HELEN KIJO BI SIMBA AMESEMA KUWA HATUA HIYO IMEFIKA BAADA YA KUMTAKA WAZIRI MKUU PINDA KUWAOMBA RADHI WANANCHI NA YEYE KUTOLUFANYA HIVYO NA WAO KUAMBUA KUCHUKUA MAONI YA WANANCHI NA KUSHAURIWA WAKAFUNGUE KESI HIYO

AMESEMA HADI KUFIKIA HAPO WAMEFIKIA HATUA YAO NZURI NA KUSISITIZA KUWA SASA WANAVIACHIA VYOMBO VYA SHERIA KUSHUGHULIKIA SWALA HILO

No comments: