Friday, October 4, 2013

KENYA HALI SIO SWARI--! GHASIA ZAZUKA NAIROBI KENYA ... VIJANA WA KIISLAM WACHOMA KANISA MOTO....

CHANZO  http://maasinda.blogspot.com/--




             Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.

            Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.

             Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.

Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.


Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.

Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa


Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.
Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.

          Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.

             Polisi ya Kenya imetangaza kuwa, watu wanne akiwemo Sheikh Ibrahim Ismail Rogo wameuawa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana ndani ya gari dogo jana usiku huko mjini Mombasa.

           Taarifa ya Polisi  ya Kenya imeeleza,  Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa mrithi wa Sheikh Aboud Rogo ambaye  naye aliuawa na familia yake kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwezi Agosti 2012.

            Mauaji ya Sheikh Ibrahim Rogo ambayo yameutikisa mji wa Mombasa, yametokea  baada ya kupita takriban wiki mbili tokea kundi la al Shabab lilipovamia  na kuua  watu wasiopungua 63 na kujeruhi mamia ya wengine kwenye jengo la maduka ya biashara la Westgate jijini Nairobi.

             Baadhi ya wananchi wa Mombasa wanakituhumu kikosi  maalumu cha kupambana na ugaidi kuwa ndicho kilichotekeleza  mauaji hayo.

          Sheikh Ibrahim Rogo ambaye alikuwa akitoa mihadhara kwenye Msikiti wa Musa mjini Mombasa alituhumiwa na jeshi la polisi kuwa anawachochea vijana wa Kiislamu kujitumbukiza kwenye makundi  ya kigaidi.

          Polisi ya Kenya imesema kuwa, Gaddafi Mohammad, Issa Abdallah  na Omar Abu Rumeisa ni miongoni mwa waliouawa, naye Salim Aboud alinusurika kwenye shambulio hilo.

No comments: