Tuesday, October 1, 2013

MCT YATANGAZA TUZO ZA WANAHABARI,YAZITUPILIA MBALI BLOG,YASEMA HAIZITAMBUI

MKURUGENZI MTENDAJI WA MCT KAJUBI MUKAJANGA AKIZUNGUMZA KATIKA UZINDUZI  HUO JIJINI DAR ES SALAAM
              Baraza la habari MCT leo limezindua rasmi mchakato wa kupata waandishi wa habari bora katika tuzo za AJAT ambazo hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu zitafanyika tarehe 14 april mwakani,katika uzinduza huo mkutugenzi wa mct amesema kuwa bado baraza lake halitambui uandishi wa habari wa kwenye mitandao kama blog na websites kwani wengi wao sio waandishi wa habari halali.

        Amesema kuwa katika tuzo hizo hazitawahusu waandishi wa habari hao wanaofanya kazi katika blog kwani hakuna chombo maaluum kinachohusika katika kuwasimamia hao.

         Amesema kuwa kama mwandishi wa blog anahitaji tuzo ni lazima afanye kazi sana na asubiri hadi pale  atakapoonekana mchango wake kwa jamii na watu wenyewe waamue kumpa tuzo na sio kusubiria kupewa na mct


KAJUBI MUKAJANGA AMBAYE NI MKURUGENZI MTENDAJI WA MCT PEMBENI YAKE NI MKURUGENZI WA TMF BW ERNEST SUNGURA

WAANDISHI WA HABARI MBALIMBALI WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO HUO

WAANDISHI WAPO MAKINI

MOJA KATI YA WAANDISHI WA HABARI JAMAL HASHIM AMBAYE MWAKA JANA ALINGARA KATIKA TUZO HIZO AKIELEZEA MCHAKATO HUO WA KUMTAFUTA MWANDISHI WA HABARI BORA

No comments: