Tuesday, October 1, 2013

SERIKALI YAENDELEA KUYAKALIA KOONI MAGAZETI ILIYOYAFUNGIA,SASA MWANANCHI MARUFUKU KUANDIKA KWENYE MTANDAO

MKURUGENZI WA HABARI MAELEZO AKITOLEA UFAFANUZI SWALA HILO MBELE YA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
              Baada ya serikali kuyafungia magazeti mawili ya kila siku ambayo ni mwananchi na mtanzania sasa imezidi kuyakali kooni baada ya leo kutangaza kiama kingine kwa magazeti hayo

        Akizungumza na waandishi wa habari jiini dar es saalaam mkurugenzi wa idara ya habari maeleo ASSA MWAMBENE amesema kuwa baada ya kufungiwa kwa magazeti hayo sasa gazeti ya mwananchi limekuwa likifanya kazi zake kwa njia ya mtandao kiti ambacho amesema ni marufuku na kuwataka kuacha mara moja mtindo huo kabla ya hatua kali hazijachukuliwa juu yao.

        Aidha katika gazeti la mtanzania amesema kuwa kampuni ya habari coperation imekuwa ikitoa gazeti la RAI kila siku sasa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo amesema kuwa gazeti hilo limesajiliwa kutoka kwa wiki mara moja ambapo amewataka kuacha mara moja mchezo huo kabla hatua kali hazijachukuliwa.

No comments: