HALI ya Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Runinga cha ITV, Ufoo Saro ambaye alijeruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzake, Marehemu Anthery Mushiinazidi kuimarika na anaweza akaruhusiwa wakati wowote baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kusafisha tumbo ambao kitaalamu unajulikana kama Toilet Surgery.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutokutajwa jina, mmoja wa madaktari katika hospitali hiyo, alisema kwa kawaida upasuaji kama huo ukifanyika kinachokuwa kinasubiriwa ni mgonjwa kupona vidonda au kupungua kwa maumivu kabla ya kuruhusiwa.
“Kimsingi hadi kufanyiwa upasuaji wa namna hiyo ni kuwa ameshatoka katika ile hali ya hatari na ameshasafishwa na kuondolewa uchafu wote uliokuwepo ikiwa ni pamoja na kumtibia vidonda vilivyotokana na shambulizi hilo,” alisema daktari huyo.
Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi alisema Ufoo anaendelea vizuri na hivi sasa ameanza kula, kufanya mazoezi kidogo na kujaribu kuzungumza, lakini bado hajaruhusiwa kukutana na watu zaidi ya ndugu wachache ambao pia wanamwangalia kwa karibu.
Msemaji wa familia ya Ufoo, Allelio Swai alithibitisha kutengemaa kwa hali ya mwandishi huyo.Swai alisema Ufoo hivi sasa anaendelea vizuri na madaktari wamewaeleza kuwa wakati wowote anaweza akaruhusiwa. MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment