MAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM AKIONYESHA PICHA YA MTUHUMIWA ABDUL THABIT MAIGA AMBAYE NDIYE MWENYE LAPTOP HIYO |
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea
kuwasaka wale wote wanahusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kifo cha
Dr. Sengondo Mvungi aliyevamiwa tarehe 03/11/2013, kujeruhiwa na kusababisha
kifo chake. Katika tukio hilo pia viliibiwa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Kompyuta ya marehemu (laptop aina ya HP).
Hadi sasa watuhumiwa waliokwisha kamatwa ni 10 ambao
tayari majina yao yalishatolewa mapema, hata hivyo katika upelelezi wa kina
imegundulika kwamba kompyuta ya marehemu inamilikiwa isivyo halali na mtuhumiwa
aitwaye ABDUL S/O THABIT MAIGA CHIEF,
umri MIAKA 20, mkazi wa VINGUNGUTI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendea kufanya jitihada
kubwa kwa lengo la kuipata “laptop” hiyo pamoja na simu moja ya marehemu. Sasa imegundulika kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu ndiye anayeimiliki
isivyo halali. Kuna dalili kuwa mtuhumiwa huyo amegundua kwamba anatafutwa hivyo anakwepa kukamatwa na anajificha maeneo
tofauti tofauti ya jiji ikiwa ni pamoja na kusafiri sehemu mbalimbali hapa nchini
kukwepa mkono wa sheria.
Laptop hiyo ni muhimu sana katika kukamilisha upelelezi
wa shauri hilo na katika taratibu za kipolisi mtuhumiwa wa aina hiyo anatakiwa
kutafutwa kwa mujibu wa PGO No 238.
PICHA YAKE NDIO HII HAPA JAMANI |
No comments:
Post a Comment