Wednesday, November 20, 2013

SAKATA LA MBUNGE IDDI AZANI KUUZA MADAWA YA KULEVYA,ALIKOMALIA GAZETI LA RAIA MWEMA KWA KUMCHAFUA,ATINGA MCT,WAHOJIWA KWA MASAA MATANO,MHARIRI WA RAIA MWEMA AKUBALI KUSHINDWA,KUMBE IDDI AZANI HAUZI UNGA

MHARIRI WA GAZETI LA RAIA MWEMA GODFREY DILUNGA AKIHOJIWA MBELE YA KAMATI YA MAADILI YA MCT
          Sakata la tuhuma juu ya mbunge wa kinondoni mh idd azani kuhusiswa na madawa ya kulevya leo limechukua sura mpya ambapo mbunge huyo amelishtaki gazeti la raia mwema la hapa tanzania kutokana na makala moja iliyoandikwa ikielezea yeye kuhusika na uuzaji wa madawa ya kulevya

          Leo makao makuu ya MCT kamati ya maadili ya baraza hiilo imewakutanisha wahusika wawili ambaoo ni mbunge IDD AZANI na mhariri wa raia mwema ambaye ni GODFREY DILUNGA na kusikiliza maelezo yao yote juu ya malalamiko hayo

         Katika malalamiko hayo mbunge aAZANI alilalalamika kuwa gazeti hilo halikumtendea haki katika makala hiyo kwani hakuitwa kuulizwa.

                          UAMUZI WA KAMATI YA MAADILI YA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) KUHUSIANA NA MALALAMIKO YA BW. IDD AZZAN DHIDI YA GAZETI LA Raia Mwema

TAREHE: NOVEMBA 20, 2013

ENDELEA HAPO CHINI----------

        Kamati ya maadili imetafakari kwa kina maandishi na maelezo ya pande zote katika shauri hili. Kamati inaamua na kutamka yafuatayo :


         Gazeti limeshindwa kuthibitishia kuwa liliongea na Mh. Azzan kabla ya kuchapa taarifa. Majibu yanayodaiwa na gazeti kuwa ya Mh. Azzan yalitoka katika chanzo tofauti bila gazeti kuongea naye ambayo gazeti lilitaka kuandika kuhusu yeye. Japo inaruhusiwa kunukuu vyanzo au vyombo vya habari vingine, ni muhimu kuvitaja vyanzo hivyo. Kama gazeti lingeongea naye huenda angeweza kutoa majibu yanayohusu mwelekeo wa stori ya gazeti lenyewe.

         Gazeti limeonyesha jitihada kubwa za kuongea na vyanzo vingi vikiwamo mamlaka mbalimbali lakini vyanzo hivyo haviwezi kuchukua nafasi ya kumhoji mutuhimiwa mwenyewe.

         Tetesi (tip) ya habari ilitoka katika mtandao na Kamati inaona hatua stahiki ya kuithibitisha Habari za mitandaoni hazikukamilishwa (was not exhausted) ipasavyo.

         Kamati inaona kuwa hakukuwa na sababu za kuchapa stori hiyo haraka kabla  ya kuongea na mhusika Azzan hata kama gazeti liliona kama running story (yaani stori inayoendelea). Hii ni kwa kuwa taarifa hii ni nyeti sana na hakuna dalili kuwa kusubiri kuichapa kungeleta madhara kwa jamii.


UAMUZI WA KAMATI


         Gazeti halikumpa nafasi stahiki Mh. Azzan katika stori yenye tuhuma nzito. Kwa hiyo Kamati inaangiza gazeti limwombe radhi Mh. Azzan kwa upungufu huo wa kitaaluma.

         Kamati inaagiza gazeti la Raia Mwema lifanye mahojiano ya kina na Mh. Azzan ili kumpa nafasi stahiki ya kujibu na kuchapisha mahojiano hayo ndani ya wiki mbili kutoka leo.

        Kamati inaagiza gazeti limfidie malamikaji gharama halisi alizoingia katika kushughulikia shauri hili.


      USHAURI


         Kamati inawakumbusha wahariri kuwa makini na kuchukua tahadhari zote za kitaaluma wanaposhughulikia tetesi (tips) zitokanazo na mitandao.


         Kamati inawakumbusha wahariri kuzingatia kanuni ya utoaji wa haki ya kujibu hasa katika taarifa zinazohusu tuhuma. Kanuni ya mizania (principle of balance) izingatiwe daima.


Mlalamikaji                        Mlalamikiwa

Jina……………………….                Jina…………………….

Sahihi…………………….                Sahihi…………………

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili


Sahihi……………………

WAJUMBE WA KAMATI HIYO WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA PANDE ZOTE MBILI
MBUNGE WA KINONDONI AKIWA MAKINI KUJIELEZA MBELA YA KAMATI HIYO

HILI NDILO GAZETI LILILOZUA MTAFARUKU

No comments: