Naibu Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya akizungumza na wadau wa sekta mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam. |
Ikiwa ni takribani
miaka 20 tangu kuasisiwa kwa Siku ya Takwimu Afrika, Serikali imesema ipo haja
ya kufanyika kwa tathmini ya ufuatiliaji wa takwimu zinazotolewa na mchango
wake katika kupanga mipango ya maendeleo
katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyowashirikisha wadau wa sekta
mbalimbali leo jijini Dar es salaam,
Naibu Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya amesema kuwa maendeleo bora huchangiwa na
upatikanaji na matumizi ya takwimu Bora zenye kuelezea uhalisia wa jamii
husika.
Amesema Tanzania ikiwa
miongoni mwa nchi zinazothamini mchango wa takwimu katika maendeleo itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa matumizi ya takwimu sahihi
yanapewa kipaumbele katika kutatua kero
mbalimbali nchini zikiwemo za ulinzi wa raia na mali zao, elimu, Afya, Kilimo
na ufugaji.
Bi. Saada amesema kuwa
kutoakana na umuhimu wa takwimu wapo baadhi ya watanzania wanaodhani kuwa
takwimu zinatumiwa na serikali pekee jambo ambalo si sahihi na kuwataka kuondoa
fikra hizo kutokana na umuhimu na mchango wake kuanzia ngazi ya familia.
“Ni vema sote tukaelewa
matumizi ya takwimu sahihi na mchango wake katika maendeleo kuanzia ngazi ya
familia pia kuondoa mtazamo kuwa takwimu zinatumiwa na serikali pekee na
kusahau kuwa takwimu zinagusa maisha ya kila siku ya watu na zina umuhimu
mkubwa sana katika kupanga mipango ya maendeleo” Amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Dkt. Albina Chuwa akizungumza kabla ya ufunguzi wa maadhimisho hayo amesema
kuwa Tanzania kama zilizvyo nchi
nyingine za bara la Afrika huadhimisha Siku ya Takwimu Afrika kwa kuwa Ofisi yake pamoja na majukumu
mengine inaendelea kuboresha na kuimarisha matumizi ya takwimu nchini.
Dkt. Chuwa amesema kuwa takwimu ni maisha ya kila siku ya mwanadamu na
zina umuhimu katika nyanja zote na kuongeza kuwa wabunge wanahitaji takwimu ili
kupanga mipango ya maendeleo ya majimbo yao, serikali nayo inahitaji takwimu
ili iweze kutekeleza mipango ya maendeleo na kutoa huduma stahiki kwa wananchi vilevile
mashirika mbalimbali yanahitaji takwimu sahihi ili yaweze kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake
mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Bw. Thomas Daniel Witz akitoa salam za Benki
ya dunia wakati wa maadhimisho hayo amesema kuwa Benki ya dunia na washirika wa
maendeleo wanatambua na kuthamini mafanikio makubwa yaliyopatikana katika
ukusanyaji na utoaji wa takwimu nchini Tanzania.
Amesema takwimu
zinazotolewa zinaongeza uwazi na uwajibikaji na kuongeza uwezo wa nchi kupanga
mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
“Napenda kuchukua fursa
hii kuipongeza Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa maendeleo na
mafanikio makubwa ya utoaji wa takwimu ambazo sasa zinaiwezesha serikali na
wadau kupanga mipango yao ya maendeleo”
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Thobias Andengenye ambaye
alikuwa miongoni mwa wachangiaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
kuhusu mchango wa takwimu katika kufanikisha majukumu ya Jeshi la Polisi
nchini. |
Naye Naibu Kamishna wa
Jeshi la Polisi nchini Thobias Andengenye ambaye alikuwa miongoni mwa wachangiaji wakati
wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini amesema jeshi la polisi linathamini mchango wa takwimu katika
kufanikisha majukumu yake. Amesema takwimu
zinalisaidia jeshi la polisi kutekeleza majukumbu mbalimbali yakiwemo ya ujenzi
wa vituo vya polisi, kurahisisha mgawanyo wa ajira kufuatana na mahitaji ya
wilaya na mikoa, uimarishaji wa mafunzo kulingana na uhitaji pamoja na kutambua
ongezeko la makosa na namna ya kukabiliana nayo katika maeneo mbalimbali
nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza kabla ya ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Amesema kuwa Ofisi yake pamoja na majukumu mengine inaendelea kuhimiza matumizi ya takwimu kutoka katika vyanzo sahihi kwa mipango ya maendeleo. |
No comments:
Post a Comment