Timu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania katika Maonesho ya ITU Telecom World
HABARI ZAIDI BOFYA HAPO CHINI----------
Tanzania inashiriki
katika Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU-International Telecommunications Union)
linalofanyika katika jiji la Bangkok nchini Thailand.
Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika Ulimwengu wa
TEHAMA, unashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio wanachama, Makampuni ya
Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano Pamoja na
Serekali, wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko makubwa
katika Sekta ya Mawasiliano.
Mabadiliko haya yanapelekea dunia kuwa na Changamoto ya Kuyakubali Mabadiliko
hayo na kukabiliana na Changamoto zake kwani faida za mabadiliko ni kubwa kwa
Jamii Habari duniani. Akizungumza jijini Bangkok, Waziri wa Mawasiliano Sayansi
na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema Tanzania iko tayari kwa na
imeshapokea mabadiliko na imetekeleza mikakati ya kuhakikisha Tanzania
inapokuwa mabadiliko bila tatizo.
Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema Tanzania inatambua umuhimu wa mabadiliko
katika TEHAMA hususan kipindi hiki cha dijitali kwani ndio njia pekee ya
kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa ufanisi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma
amesema Tanzania tayari mstari wa mbele kuhakikisha inachochea mabadiliko
ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili wananchi wafaidike na huduma za
Mawasiliano. "Tuna mfumo mzuri wa usimamizi wa leseni za muingiliano wa
teknolojia, sheria na kanuni nzuri ambazo zinawezesha mabadiliko katika TEHAMA
kunufaisha watanzania. Tayari Tanzania imeingia katika mfumo wa Utangazaji wa
digitali na tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwepo kwa huduma nyingi
zaidi kurahisisha maisha ya watanzania". Amesema Profesa Nkoma.
Taasisi kadhaa toka Tanzania zinashiriki Kongano hili kutoka Tanzania ikiwa ni
pamoja na W ziara ya Afya, Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia, DTBi
ya wavumbuzi na wagunduzi, NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa, MaxCom.
Kongano hili linafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 19 - 22 Novemba 2013.
Tanzania inashiriki na kauli Mbiu ya nchi "Tanzania: Africa Strategic ICT
Hub". Pamoja an Kongano pia yako Maonesho ya ICT yenye nia ya kuonesha
jinsi nchi zinavyochochea maendeleo kwa raia wake kupitia TEHAMA. Banda la
Maonesho la Tanzania limevutia watu wengi wanafikia kujifunza jinsi Tanzania
imeweza kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na jinsi wananchi wanafaidika na
huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.
Aidha Baadhi ya Taasisi zinazoshiriki zinaangalia uwezekano wa kuchochea zaidi
upatikanaji wa huduma zao kwa kuwa na washirika katika shughuli zao. Leo
asubuhi Ujumbe wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano Maalum wa Wawekezaji
Katika Sekta ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu Katibu Mkuu wa ITU Bwana
Houlin Zhao.
|
|
No comments:
Post a Comment