Na Karoli Vinsent
BAADHI ya
Watanzania wameficha mabilioni mengi ya fedha katika visiwa vya Jersey
vilivyopo barani Ulaya, kuliko hata mabilioni yaliyobainika kufichwa katika
benki mbalimbali nchini Uswisi, Habari 24 limeambiwa.
ENDELEA KISOMA HAPA----
Taarifa
mpya ambazo blogs hii imezipata kutoka Uingereza zinaeleza kwamba fedha za
Watanzania pekee zilizoko katika visiwa hivyo zinakadiriwa kufikia kiasi cha
pauni za Uingereza milioni 413 (sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.06).
Fedha
hizo zinatosha kuhudumia bajeti za wizara za Afya, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Afrika Mashariki kwa mwaka mzima bila ya
kuomba fedha kutoka kwa wafadhili na bado ‘chenji’ ikabaki.
Blogs hii
haiwezi kutaja chanzo cha habari hizi kwa vile taarifa hii ilipatikana katika
mkutano uliofanyika Uingereza wiki iliyopita chini ya kanuni za Chatham (Chatham
Rules) ambazo zinakataza kutaja vyanzo vya habari zilizopatikana kutoka
katika mikutano inayotawaliwa na kanuni hizo.
Kwa mujibu
wa taarifa za uhakika zilizopatikana, habari24 limeelezwa kwamba zaidi
ya Jersey, kuna fedha nyingine nyingi katika visiwa vingine kama Cayman na Isle
of Man ingawa pia kuna fedha zilizohifadhiwa jijini London, mji mkuu wa
Uingereza.
“Kuna
watu binafsi ambao wamehifadhi fedha zao. Kuna fedha za kampuni kadhaa na kuna
fedha za inayoitwa mifuko ya hisani. Naweza nikashindwa kuwapa majina haswa ya
wenye fedha hizo lakini nadhani inawezekana kuwapa majina ya kampuni na mifuko
hiyo ya hisani (trusts), kilieleza chanzo hicho.
Kisiwa
hicho ni miongoni mwa nchi zinazopendwa na watu, kampuni au taasisi zinazokwepa
kulipa kodi au zinazopata mapato yake kwa njia ya kifisadi kwa vile zinatoza
kodi kidogo na zina sheria zinazolinda usiri wa walioweka mali zao.
Mkutano
huo ulielezwa kwamba visiwa hivyo vilivyo chini ya Uingereza lakini
vinavyojitawala vyenyewe vimehifadhi kiasi cha pauni bilioni 40 kutoka Afrika
na katika hizo, pauni milioni 413 zinatoka Tanzania.
Visiwa
vya Jersey vilijipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania miaka michache iliyopita
baada ya kubainika kwamba aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew
Chenge, alikuwa na akaunti katika visiwa hivyo ambayo ndiyo iliyotumika
kumwekea fedha (dola milioni moja) zinazodaiwa kutokana na mauzo ya rada ya
kampuni ya BAE Systems kwa serikali ya Tanzania
No comments:
Post a Comment