Wednesday, November 13, 2013

KIFO CHA DK MVUNGI CHAZUA MAKUBWA,MBATIA ATANGAZA RATIBA YA MSIBA,KOVA NAYE AJA NA MWINGINE AMBAYE ANAHUSIKA KUMUUA.ASEMA POLISI HAILALI HADI WASHIKWA WOTE

MWENYEKITI WA NNCR MAGEUZI JAMES MBATIA AKIZUNGUMA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM KUHUSU KIFO CHA DK MVUNGI
      Kufwatia kifo cha aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba tanzania na pia kiongozi wa nccr mageuzi EDMUND SENGONDO MVUNGI chama cha nccra kimetoa taarifa rasmi ya msiba huo na ratiba rasmi.

            Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam mmwenekiti wa nccr mageuzi JAMES MBATIA asmesema kuwa mwili wa marehemu utawasili siku ya ijumaa ya wiki hii ambapo utaagiwa katika kanisa la mtakatifu joseph alafu kupelekwa ukumbi wa karimjee jijini dar es salaam kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali.baada ya hapo mwili utalazwa nyumbani kwake siku ya jumamosi kibamba alafu jumapili utasafirishwa kupelekwa mwamga kilimanjaro kwa ajili ya maziko


MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI

KAMANDA KOVA AKIONYESHA BAADHI YA MILIPUKO AMBAYO MHALIFU HUYO AMEKAMATWA NAYO JANA USIKU JIJINI DAR ES SALAAM
     Katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam limetangaza kumkamata mtuhumiwa wa kumi ambaye alihusika katika kumshambulia dk MVUNGI kwa mapanga na kumsababishia kifo chake.

     Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam kamishna wa polisi kanda maalum ya dar es saslaam SULEMAN KOVA amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye kwa jina ni JOHN MAYUNGA mkazi wa kiwalani jijini dar es salaa alionekana na wasamaria wema jana usiku katika kibanda kimoja cha kuonyeshea video ntaa wa twigwa jangwani ambapo polisi walifika na kumkamata na kwenda nayew hadi anakoishi ambapo walifanikiwa kuumkamata na bunduki moja ambayo iuliibiwa nyumbani kwa dk mvungi,pamoja na miulipuko mbalimbali ambayo wanaitumiaga katika uhalifu wao

        Kamishna amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na uhalifu nyumbani kwa dk mvungi ambapo piua imegundulika kuwa alikuwa mfungwa aliyewahi kufungwa miaka saba na kisha kuachiwa.
NA HII NDIO BUNDUKI AMBAYO ILIKUWA KWA DK MVUNGI AMBAYO AMEKUTWA NAYO MHALIFU HUYO



No comments: