KAMANDA WA POLISI KINONDONI CAMILLIUS WAMBURA .PICHA NA MAKTABA |
Na Karoli Vinsent
JESHI la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Limeanza msako makali kuwasaka watu waliousika na mauaji ya Dereva wa Gari la shirika la utangazaji Tanzania Tbc.
Hayo yamesemwa leo na kamanda wa polisi, mkoa wa kipolisi wa kinondoni Camillius Wambura Amesema kwa sasa wameanza msako makali kuwasaka watu wanaosadikia kuwa ni Majambazi waliousika kwenye mauaji ya Dereva wa Gari wa Shirika la Utangazaji la Taifa Tbc Ramadhani Gize.
Kwa mujibu wa kamanda wa Wambura alisema tukio hilo lilitokea siku ya tarehe 5-11 2013 majira ya saa nne kasoro usiku huko maeneo ya ubungo Maziwa katika Manispaa ya kinondoni ambapo majambazi wawili wakiwa na silaha (bunduki) walivamia katika Duka liitwalo Namanga Shoping Center linalomilikiwa na mtu aitwaye Camdan Rajabu, miaka 45 mkazi wa ukonga Mombasa
Wambulla anasema majambazi walipovamia walimtishia kwa hiyo silaha na kupora pesa taslim kiasi bado akijajulikana pamoja na vocha zenye thamani ya laki nne, wakati wanafanya ujambazi ndani ta duka hilo nje Marehemu alikuwa kwenye gari aina STK 335 Toyota Land Cruiser mali ya shirika la utangazaji la Taifa Tbc lilokuwa limegeshwa nje ya eneo la tukio.Wakati Marehemu anatka kuondoka na Gari yake ndipo Jambazi aliyekuwa nje ya duka hilo alifyatulia marehemu risasi ya kichwani na kupelekea Mauti.
Aidha kamanda wambura ameomba wananchi kutoa taharifa juu ya watu walio usika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment