Na Karoli Vinsent
SHIRIKA lisilo la Kiserikali la
Action Aids Linalohusika na maswala ya Utafiti ndani na nje ya Tanzania
Limetaka Serikali ya Tanzania kuwaambia watanzania jinsi ya matumizi ya kodi
wanazokusanya kutoka kwa wananchi.
Hayo yalisemwa leo jijini Dar es
salaam na Mkurugenzi wa tasisi hiyo, Wamilika Gama alitaka Serikali ya
Tanzania kuwaambia wananchi juu ya mtumizi ya Kodi wanayokusanya kutoka kwa
wananchi.
“Tunaiomba serikali watuambi sisi
wananchi matumizi ya kodi wanayokusanya kutoka kwa wananchi maana
tunahakia ya kuuliza kwasababu tunaoa kodi atujui zinafanya nn maana kodi
nyingi zinakusanywa kilia kona ila sisi wananchi awatuambii wanafanyia
nn?”alihoji Gama
Vilevile mkurugenzi huyo alishangaa
wananchi watanzania kukaa kimya kuhusu suala hili la kodi
“kuna kodi zinakusanywa kwenye
vijiji kule ila akuan wananchi anayehoji kodi hizi zinafanya nn,na leo
mwananchi akihoji ataonekana mtu wa ajabu sana,lakini anahaki ya kuhoji kama
mwananchi kwakuwa yeye ndio ,mlengwa mkubwa”alimalizia Gama
Kwa upande wake Ofisa Mipango wa
taasisi hiyo Stivin Alocye,naye aliitaka serikali ya Tanzania kuacha kumtwisha
mzigo mwananchi kwenye kodi badara yake wangeegemea zaidi kwenye mashirika
zaidi na taasisi binafsi pamoja na makampuni ya simu amayo yamekuwa yakipata
faida nyingi huku Serikali haiambulii kitu
NDUGU MSOMAJI TUNAOMBA RADHI KWA HABARI AMBAYO HAINA PICHA
No comments:
Post a Comment