Mzee Nelson Mandela (katikati) akisaidiwa na rais Jacob Zuma kushoto na Winnie Mandela katika picha ya hivi karibuni.
CAPE TOWN.
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela anapumua bila ya msaada wa mashine ingawa hawezi kuzungumza kwa sasa.
Mke wa zamani wa kiongozi huyo, Winnie
Madikizela-Mandela aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), kuwa
Mandela yuko chini ya uangalizi wa madaktari 22.
Winnie alisema kiongozi huyo anasumbuliwa na homa ya mapafu.
Alisema Mandela hawezi kuzungumza kwa kuwa amewekewa mipira mdomoni ili kuondoa maji kwenye mapafu yake.
“Kwa kweli hawezi kutamka neno lolote, pia sauti
yake imekauka. Anawasiliana kwa ishara zaidi. Madaktari wanaamini sauti
yake itarudi,” alisema.
Winnie alisema Mandela hivi sasa anatambua watu
kitu ambacho kinawapa moyo. Kiongozi huyo wa kwanza mweusi Afrika
Kusini, aliruhusiwa kutoka hospitali, Septemba Mosi, mwaka huu baada ya
kulazwa kwa miezi mitatu.
Awali, Winne alikanusha madai kwamba mumewe huyo
wa zamani alikuwa akiendelea kupumua kwa msaada wa mashine: “Nimesikia
hizi taarifa kuwa Mandela anapumua kwa mashine. Habari hiyo si ya
kweli.”
“Hivi sasa mkazo mkubwa ni kuhakikisha kuwa
Mandela anawekwa katika hali ya usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha
hadhuriwi na vijidudu vya magonjwa mbalimbali. Chumba chake ni kama
Chumba cha Wagonjwa Mahututi cha Hospitali (ICU).”
Mandela, ambaye alitumikia kifungo cha miaka 27 jela kabla ya kutoka na kuendeleza harakati za kudai haki kwa wote Afrika Kusini, alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo mwaka 1994
No comments:
Post a Comment