SAKATA la Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya (CCM) kudaiwa kumbaka mwanafunzi na kumtishia kumuua, linazidi kuchukua sura mpya ambapo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto wamengilia kati.
ENDELEA HAPA CHINI-------
Baada Gazeti moja la kilia siku kuliripoti kauli ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuwa watamchukulia hatua Kapuya mara moja baada ya mtoto huyo kuandikisha maelezo na kuwasilisha vielelezo polisi.
Wakati hali ikiwa hivyo, huku chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) nacho kikijinasua na kutaka Kapuya abebe mzigo wake mwenyewe, Blogs hii limedokezwa kuwa IGP Mwema tayari ameingilia kati na kumwagiza Kamishna Kova kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa haraka.
Chanzo hicho kilidokeza kuwa IGP amelazimika kuingilia kati baada ya kufuatwa na Naibu Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, aliyetaka kujua ni kwanini mtuhumiwa hachukuliwi hatua baada tuhuma hizo kufichuliwa.
Taarifa za ndani zilidokeza kuwa serikali sasa inaendelea na utaratibu wa kumwandalia Prof. Kapuya mashitaka ya ubakaji na kutishia kumuua mwanafunzi huyo wa miaka 16.
Kwa siku tatu mfululizo Blogs imeripoti madai ya mtoto huyo aliyedaiwa kubakwa na Prof. Kapuya, ambaye pia amewahi kushika nafasi za uwaziri katika wizara mbalimbali.
Kwa mujibu wa ujumbe mfupi wa maandishi ya simu (sms) ambao gazeti hili linao, Prof. Kapuya kupitia namba iliyosajiliwa kwa jina lake alitishia kumuua mtoto huyo na dada yake akitamba kuwa serikali hii ni yao haiwezi kumfanya kitu.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema nchi imefika pabaya kama viongozi wanaweza kutoa vitisho na tambo za watoto wao kuuza dawa za kulevya, huku vyombo vya dola vikishindwa kuchukua hatua.
Sitta ambaye pia ni spika mstaafu na Mbunge wa Urambo Mashariki, alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika mahafali ya 15 ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Agape Seminari iliyoko Marangu, wilayani Moshi vijijini.
Alisema kuwa nchi imegawanyika kimakundi, ambapo baadhi ya viongozi wamekuwa na kiburi cha kutamba kwamba hawawajibiki kwa vyombo vya kisheria.
Sitta alitolea mfano kitendo cha waziri mstaafu ambaye sasa ni mbunge, aliyeripotiwa na vyombo vya habari akidaiwa kumtisha mtoto aliyemtuhumu kuwa alimbaka mara mbili alipoitwa kwake kuchukua ada.
Katika moja ya ujumbe wa maandishi (sms), mbunge huyo ambaye Waziri Sitta alimtolea mfano, anatamba na kumtisha binti huyo kuwa atamuua huku akihoji: “Watato wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapigana nasi?”
Sitta alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi kubwa, hivyo haiwezi kuendeshwa hovyo hovyo, na kwamba lazima iendeshwe kwa viwango vya maadili vitakavyoleta maendeleo.
Wachambuzi wa masuala ya mambo wanainyoshea mkono jeshi la Polisi nchini
kushindwa kumchukia hatua Waziri huyo mstaafu kutokana na kitendo chake cha
kinyama alichomfanyia moto huyo huku wengine wakihoji jeuli hiyo anaitoa wapi?
Kwa mujibu wa wananchi walio zungumza na Blogs
wamemtaka Rais kikwete kuingila kati na kukemea unyama uliofanywa na mbunge
huyo na kumchukulia hatua kali za kisheria na wanachi wakaenda mbali zaidi
wakilifananisha tukio hilo alilofanya Kapuya la kumbaka mwanafunzi na
kumwambukiza virusi na lile lilofanywa
na msanii wamuziki Nguza Viki na wanae,
Kitendo hiko kilipelekea kuhukumiwa kifungo cha maisha
wananchi wanashangaa kwann Serikali serikali inashindwa kumkamta kapuya?Huku
kukiwa na Ushahidi wa wazi kabisa
No comments:
Post a Comment