Thursday, November 14, 2013

PICHA :- TUKIO ZIMA LA KUKAMATWA KWA DAKTARI MSTAAFU AWAKITOA WANAWAKE MIMBA HUKO MOSHI

          JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kumnasa daktari mstaafu wa hospitali ya rufaa ya Mawenzi,mkoani Kilimanjaro, Frances Shayo(56) akiwa katika harakati za kuwatoa mimba wanawake wawili akiwemo Irene Musa(18) mwanafunzi wa shule ya sekondari Nkwereko iliyoko Masama wilayani Hai.

   Daktari huyo ambaye anatajwa kufanya vitendo hivyo mara kwa mara amekamatwa pamoja na watu wengine watano wakiwa katika nyumba ya mkazi wa Kata ya Ng’ambo aliyefahamika kwa jina moja na Minde.

     Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema daktari huyo amekuwa akifanya shughuli hiyo kwa muda mrefu katika eneo hilo na mara nyingine amekuwa akifanya shughuli za kuwatairi watoto katika nyumba ya rafiki yake huyo.

     Akizungumza na waandishi wa habari daktari Shayo amesema msichana huyo alifika katika nyumba hiyo akiwa na tatizo la kufunga kutokwa na damu hivyo alikuwa kwenye harakati za kutaka kumsaidia . 

      Kwa upande wake mama mzazi wa binti huyo,Rozi Urasa amesema alifika nyumbani kwa daktari huyo baada ya kushauliwa na baadhi ya ndugu zake kumpeleka kutoa ujauzito huo kutokana na kwamba huenda binti huyo akakosa kazi pindi atakapokuwa akitafuta kazi akiwa na ujauzito

                                    PICHA KATIKA TUKIO HAPO CHINI

Askari polisi wakiwa na silaha wakiwa wamezingira nyumba iliyokuwa ikitumika kwa shughuli za kutolea Mimba



Daktari mstaafu wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi Frances Shayo akiwa mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya kumkamata akitaka kuwatoa mimba wasichana wawili.

Mmoja wa wanawake waliokutwa katika nyumba hiyo wakidaiwa kumsindikiza binti mmoja ambaye ni mwanafunzi kwenda kwa daktari huyo kutoa ujauzito.


Msichana Irene Musa ambaye anadaiwa kuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Komkwa Masama wilayani Hai akitolewa kwenye nyumba ambayo anadaiwa kwenda kutolewa ujauzito .


Mmoja wa wanawake waliokutwa katika nyumba hiyo akidaiwa kwenda kutoa ujauzito kwa daktari huyo.


mati wa watu waliofika katika nyumba ambayo inadaiwa kufanyika vitendo vya kutoa mimba. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

No comments: