Thursday, November 21, 2013

TUJITOKEZE KUWACHANGIA WALEMAVU---YUSUPH MWENDA

                             Manispaa ya kinondono sasa imekuwa mfano wa kuigwa katika manispaa zote nchini baada ya kuanzisha zoezi la kuwajali wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa kufanya mchango wa kuwanunuia vifaa mbalimbali ikiwa na lengo la kuwasaidia ili waweze kupata elimu iliyo bora sawa na wanafunzi wengine ambao hawana ulemavu
          Akizungumza na HABARI24 BLOG ofisini kwake meya wa manispaa ya kinondoni  YUSUPH MWENDA amesema kuwa nia na madhumuni ya manispaa katika mpango huo ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye ulemavu wanapata fursa ya kusoma na kujiendeleza kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ili kuwezesha ursa ya kuibua vipaji vyao.
      Amesema kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo na mitazamo hasi katika jamii juu ya watoto wenye ulemavu mpaka kufikia wazazi wengne kuwaficha ndani kwa lengo la kuogopa jamii inayowazunguka jambo amblo amesema kuwa sio sawa kabisa kufanya hivyo na ndio maana manispaa hiyo sasa imeamua kulivalia njuga swala hilo
        Manispaa ya kinondoni ina wananfunzi wenye ulemavu zaidi ya 1800 katika shule mbalimbali za msingi na sekondary ambapo wanafunzi huwa wanahitaji vifaa maalum vya kujifunzia kama fimbo nyeupe,na mashine z kuandikia,shemisikio kwa walemavu wa kusikia,miwani,mafuta na lotion kwa wlemavu wa ngozina viungo pamoja na vitabu na karatasi
      Meya wa kindondoni anawataka wtu mbalimbali wenye uwezo na wasio na uwezo wajitikeze kwa wingi katika kuchangia walemavu hao.
JINSI YA KUCHANHIA NI---
M-PESA--0768727314
 TIGO PESA--0712200022
ACOUNT NAMBA---22610001899 ELIMU MAALUM KINONDONI
AU PELEKA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA KINONDONI IDARA YA ELIMU

No comments: