Na Karoli Vinsent
Hali ya kisiasa ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema imefikia pabaya baada ya kumvua uwongozi wa juu Zitto Kabwe.
endelea hapo----------
Zitto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,ikumbukwe mwanzoni mwa
Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na
Lema kuwa anakataa posho za
vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali
Dar es Salaam. Suala la
hatma ya Naibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe
ndilo lililotawala katika siku ya pili ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho
na kusababisha mvutano mkali miongoni mwa wajumbe.
Pamoja na ukweli kuwa kulikuwa na ajenda kadhaa zilizokuwa
zimepangwa kujadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika Dar es
Salaam, suala la Zitto ndilo lililochukua muda mrefu zaidi kujadiliwa.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho ambayo
imeifikia habari24 kuwa kikao hicho zilieleza kuwa wajumbe waligawanyika
makundi mawili, baadhi wakipendekeza Zitto avuliwe nafasi yake ya Naibu Katibu
Mkuu kwa maelezo kuwa anakwenda kinyume na taratibu za chama hicho na wengine
wakipinga hatua hiyo kwa maelezo kuwa haina tija.
Mpaka saa moja usiku jana jioni ambapo habari 24 ilizipata
ni kuwa kikao hicho kilikuwa bado kikiendelea na suala hilo lililokuwa
chini ya ajenda ya hali ya siasa nchini.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa chama hicho,
Benson Kigaila aliahidi kuwa taarifa rasmi ya kikao hicho ingetolewa baadaye na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Tuhuma za Zitto
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwanzoni mwa
Novemba mwaka huu aliingia katika malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema kuhusiana na masuala ya posho, akituhumiwa na Lema kuwa anakataa posho za
vikao bungeni, lakini anapokea posho kutoka mashirika mbalimbali nchini.
Pia, aliingia katika malumbano na chama chake baada ya
kutumia kofia yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kauli ambayo jana Kigaila aliitolea ufafanuzi na kueleza
kuwa Chadema kimekaguliwa na hesabu zake tayari zipo kwa Msajili wa Vyama vya
Siasa.
Hekaheka za jana
Mvutano wa jana ulianza baada ya Mbowe kufungua kikao hicho
saa 4:00 asubuhi.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilizoifika habari 24
zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe, wakiwamo wabunge, walitaka Zitto
avuliwe nafasi aliyonayo na kuwa mwanachama wa kawaida, huku wengine wakipinga
hatua hiyo kwa maelezo kuwa Zitto hakuwepo katika kikao hicho na kwamba
alipaswa kusikilizwa.
“Baada ya hali kuwa hivyo, Mbowe alipendekeza kuwa Zitto
asijadiliwe kwa kuwa hakuwepo katika kikao hicho,” kilieleza chanzo cha habari
hizo.
Zitto alikuwa katika safari ya kikazi huko Sudan Kusini
akiwa amefuatana na wajumbe wa PAC.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Zitto alitafutwa na alituma
salamu kwa wajumbe wa kikao hicho akiwaeleza kuwa alikuwa njiani na kuahidi
kuwa angehudhuria mara tu baada ya kuwasili.
“Zitto alituma ujumbe kuwa anakuja katika kikao, kilikuwa na
ajenda nyingi lakini suala lake lilijadiliwa kwa kirefu sana,” kilieleza chanzo
chetu. Licha ya ombi la Mbowe, bado wajumbe walishinikiza kuendelea kumjadili
Zitto hivyo ni kusababisha kuchelewa kujadiliwa kwa ajenda nyingine.
Tangu juzi, siku ya kwanza ya kikao hicho, ulinzi
uliimarishwa nje ya Jengo la Ubungo Plaza na jana walinzi wa chama hicho, Red
Brigade waliwatimua waandishi wa habari waliokaribia eneo hilo wakisema hayo ni
maagizo kutoka kwa uongozi wa juu.
Yaliyojadiliwa
Katika ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari jana jioni,
Kigaila alisema kikao hicho kilichoanza juzi, kimejadili mambo mbalimbali.
Alisema juzi kikao hicho kilijadili muhtasari wa vikao viwili vya dharura vya
Kamati Kuu vilivyofanyika hivi karibuni.
“Tumejadili taarifa ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la
Kiembesamaki, Zanzibar unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni... tunathibitisha
kuwa tutashiriki,” alisema.
“Kulikuwa na taarifa ya hesabu za chama zilizokaguliwa na
kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na taarifa za fedha za utendaji
kuanzia Kamati Kuu iliyopita mpaka Kamati Kuu ya sasa,” alisema Kigaila.
Huku akionyesha kitabu cha ukaguzi wa fedha mwaka 2010/11 na
2011/12 alisema: “Kamati Kuu imeridhika kuwa chama kimekaguliwa na hatuna deni
kwa msajili.
Ajenda za jana
Alisema kikao cha jana kilijadili ajenda za uboreshaji wa
jengo la makao mkuu pamoja na kupanga upya kurugenzi za chama hicho pamoja na
nguvu kazi ya makao makuu ili kuweza kutekeleza vizuri majukumu yake.
“Ajenda inayoendelea hivi sasa ni ya uundaji wa programu ya
`Chadema ni Msingi’, ambayo lengo lake ni kukijenga chama katika ngazi za chini
kabisa. Huu ni mpango mkuu wa chama wa `Vuguvugu la Mabadiliko’ (M4C). Ajenda
ya mwisho itakuwa ni kujadili hali ya kisiasa nchini.”
Zitto atinga usiku
Zitto alifika katika kikao hicho jana saa 2.24 usiku akiwa
na walinzi wanne na habari kutoka ndani zinasema kwamba mara baada ya kuingia,
ajenda ya kumjadili ilirejea. Ilielezwa kwamba alipewa nafasi ya kujitetea
baada ya kusomewa ‘mashtaka’ yaliyokuwa yakimkabili.
Mwandishi wa blog hii aliyekuwa katika eneo hilo anasema
baada ya kurejeshwa kwa agenda hiyo malumbano makali yalizuka kwani wajumbe
walikuwa wazungumza kwa sauti za juu na jazba kiasi
Huku wakikosa imani na Zitto Kabwe kwa kitendo chake
cha kukisariti chama hicho,kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari
kilichopo ndani ya mkutano huo jana kilisema ajenda ya kumfukuza Zitto Kabwe
jana ilikuwa ukitawala na kufikia hatu ya kifika hatua ya kumvua uongozi wa
chama hicho na pia na kutaka apewe siku kazaa kwann asivuliwe uwana chama wa
chama hicho.
Uchunguzi uliofanywa na Habari24 umebaini, uwenda yale
yalioandikwa kwenye wakala uliosambazwa kwenye mitandao juu ya hujuma
anayofanya zitto kabwe na kushikiliana na baadhi ya maofisa wa usalama wa
taifa kuhusu kukiujumu chama hicho uwenda ikawa sababu iliyowafanya baadhi ya
wajumbe wa mkuto huo kumfukuza zitto kabwe,
Ikumbukwe baada ya kusambaa kwa walaka huo kwenye mitandao
ya kijamii wenye kichwa cha habari walaka wa siri kuhusu Zitto kabwe,Zitto
kabwe mwenyewe aliibuka na kuupinga walaka huo na baadhi ya viongozi wa chadema
pia waliupinga walaka huo wakisema huwenda ni ujuma za baadhi ya watu
wasiokitakia jema chama hicho.
Katika hari ya kushangaza mwandishi wa blogs alishuhudia
kwenye mitandao wa kijamii amabapo uliwekwa walaka huo, katika hali ya
kushangaza baadhi viongozi wa chama cha chadema waaliweka alama ya ku like kama
kuunga mkono yale yalioandikwa kwenye walaka ule na pia jambo jingine walaka
ule ulichapishwa kwenye blog ya kiongozi wa chadema na jina tunalo
tunaliifadhi na kutia mashaka kuhusu ukweli walaka huo
Habari hii imeandikwa na Karoli vinsent pamoja na
kushirikiana na Gazeti la mwananchi pamoja na vyanzo mbalimbali ndani ya
chadema
No comments:
Post a Comment