PICHA NA MAKTABA |
NA KAROL VICENT ------ CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) kimemtaka Rais Jakaya kikwete kuwatimua malamoja moja mawaziri mizigo kwa kushindwa kuwatumikia
wananchi na Kuendesha Siasa za umangi meza.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa itikadi na
uwenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, makao
makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam,Nape alisema kamati kuu ya chama cha
mapinduzi ya CCM imefikia maamuzi ya kumtaka Rais Kikwete kuwafukuza kazi
mawaziri hao kutokana na kutowatumikia wananchi na kuendesha Siasa za Umangi
meza katika wizara zao.
ENDELEA KUSOMA HAPO CHINI--------
“Kamati kuu
ya CCM iliyokaa imemtaka Mwenyekiti wa chama chetu,Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua mawaziri saba
mizigo kutokana na kushindwa kuwatumikia wananchi na kuendesha siasa za umangi
meza,haya maamuzi hatusemi sisi kama viongozi wa kamati kuu,bali maamuzi hayo
yanatokana na vilio vya wananchi”.alisema Nape
Nape,aliwataja
Mawaziri hao mizigio kuwa ni profesa Jumanne Maghembe ambaye ni waziri wa Maji,Waziri
wa Kilimo,Chakula na Ushirika Christofa Chiza,Waziri wa elimu na Ufundi Shukuru
Kawambwa,Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia,Waziri wa Viwanda na Biashara Abdara
kigoda.
Kuhusu
waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika christofa Chiza
Nape,alisema Waziri huyo ameonyesha
kushindwa waziwazi kuongoza wizara hiyo
kwa kitendo tangu hawe Waziri wa kilimo, katika kipindi cha miaka mine ya
uwongozi wake hajawai kwenda kwenye Bohari ya Chakula ya Taifa iliyoko mkoani
Ruvuma.
“Waziri huyu
tangu hawe waziri wa Kilimo hajawai kwenda kwenye ghala la chakula kule mkoani
Ruvuma,lakini Ukiangalia katika Safari zake za kwenda nje ni nyingi zaidi
kuliko zile ambazo makurima ananufaika,na jambo jingine ni Waziri huyo
kushindwa kuvisimamia vyama vya Ushirika ambavyo vimekuwa vikiwaibia wakulima”alizidi
kufafanua Nape
Vilevile
Nape akafafanua kuhusu kilio cha
wakulima ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu kukosa mbolea kwa wakati,sababu kuu
imetokana na Udhaifu wa uongozi wa Waziri huyo.
Kuhusu Waziri wa elimu na Ufundi Shukuru
Kawambwa
Nape alisema Waziri huyo ameshindwa
kuisimamia wizara hiyo, kutokana kuzidi madai ya mshahara walimu pamoja na madeni na kupandishwa madaraja,
Kuhusu Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia,
Katibu huyo mwenezi na itikadi
alisema,Waziri huyo ameonyesha kushindwa kuongoza Wizara hiyo kutokana na
Ufisadi wa Mabilioni ya Fedha zinazopotea kwenye Halmashauri mbalimbali hapa
nchini huku watu wanaofanya ufisadi huo wakifumbiwa macho tena wanahamishwa
kutoka Halmashauli moja kwenda nyingine.pasibo kuchukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment