KAMANDA WA UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE ASP RENATUS CHALYA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO OFISINI KWAKE.
Na karoli Vinsent
MIEZI michache kupita Tangu
waziri wa uchukuzi dokta Harisoni Mwakyembe kufanya mabadiliko kwenye uwanja wa
kimataifa wa Uwanja wa ndege wa Mwalimu JK NYERERE ,watu wa wawili wamekamatwa
wakisafirisha madawa ya kuleva.
ENDELEA HAPO CHINI--------
Hayo yamethibitiswa leo na kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa
JK NYERERE Asp Renatusi Chalya,wakati akizungumza na wandishi wa
habari.Alithibitisha kukamatwa kwa wanawake wawili ambao walikuwa wakijalibu
kusafirisha madawa kutoka Tanzania kwenda China,
Chalya,amesema wanawake hao walikamatwa jana tarehe 11 majira ya saa
kumi na mbili usiku wanawake aliwataja kwa majina kuwa Mariam Hamadi umri wa
miaka 29 kabira ni Mhehe, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam ambaye paspoti
yake ni Ab,576285,pamoja na mwenzake Khadija Abduli umri miaka 30 kabira ni
Mnyamwezi makazi wa Tabata Kisukulu Jijini Dar es Salaam.
Kamanda Chalya alisema watuhumiwa hao
walikuwa wanataka kusafiri na shirika la ndege la Quatal ndipo
askari waliokuwepo uwanjani walipowatilia shaka Abaria hao ,Na kuanza
kuwanawabana pamoja na kuwapekuea ndipo Mariam Hamadi alikubari kuwa amemeza
kete 72 za madawa ya kulevya,mpaka mda huu alikuwa ametoa kete 22 kutoka
tumboni mwake.
Katika hali ya kushangaza Mtumiwa wenzake
Khadija Abduli alikataa kubeba madawa ya kulevya na kusema yeye alikuwa
anamsindikiza rafiki yake ambae ni Mariam.Katika kuonyesha umakini kwa polisi
waliokuwepo uwanjani hapo wakazidi kumbana ndio wakagundua alikuwa na kete 122
na yeye kuzitoa kete hizo alizokuwa amezimeza tumboni mwake.
Katika hatua nyingine kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Juliusi Kambarage Nyelele Asp Renatusi Chalya amesema jana jeshi hilo
la polisi,majira ya saa 7 mchana,jehi hilo la uwanjani hapo limemkamata
mtu mmoja mbaye ni Raia wa China, bwana Guyan Juhim mwenye paspoti yenye
namba T609987,ambapo mtu huyu alikamatwa na Madini kilo 82 ambapo alikuwa
anayasafilisha kinyume na taratibu.
Vilevile Kamanda Chalya amewahasa wananchi kwa kuwataka wafanye kazi
zingine kuliko biashara chafu za Madawa ya kulevya kwa kuwa hazina tija na wala
hazijengi,na kusema kwa sasa jehi hilo la polisi kitengo cha uwanja wa ndege
limejipanga kukabiliana na biashara hizo chafu ambazo zimekuwa zikiitia nchi
aibu kubwa katika medani za kimataifa.
|
No comments:
Post a Comment