Na karoli Vinsent
WAKATI mazingira ya mgogoro uliopo ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kusimamishwa uongozi kwa Naibu
Katibu Mkuu wake, Kabwe Zitto na mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo
yakielekeza umma kujiuliza kama chama hicho ni sikio la kufa kwa sasa, vyama
vitatu vya siasa hapa nchini vimemkaribisha mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini
(CHADEMA), Zitto , kujiunga navyo endapo atafukuzwa katika chama chake
cha sasa, Habari24 imebaini.ENDELEA ZAIDI HAPA -----
Taarifa hii mpya inakuja katika kipindi ambacho chama hicho
kikuu cha upinzani nchini kikiwa, katika mgogoro mkubwa zaidi kuwahi
kukikuta tangu kilipoanzishwa miaka 20 iliyopita.
Mwandishi wa Blogs alizungumza na baadhi ya viongozi
wa vyama hivyo na wamethibitisha kwamba wako tayari kumpokea mwanasiasa huyo,
endapo chama chake kitamfukuza kama dalili zinavyoonyesha kwa sasa.
Kamati Kuu ya CHADEMA imempa Zitto na mjumbe wa kamati hiyo,
Dk. Kitila Mkumbo, muda wa siku 14 kuanzia Ijumaa iliyopita wajieleze kwa nini
wasifukuzwe kutoka kwenye chama hicho kutokana na kutuhumiwa kufanya uhaini.
Vyama ambavyo Habari24 inafahamu kuwa viko tayari kumpokea
Zitto ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Wananchi (CUF) na chama cha
NCCR-Mageuzi; ambavyo pia ndiyo vyama vinara kwa siasa za hapa nchini, kama
ilivyo kwa CHADEMA.
Ingawa jitihada hizo hazijawa rasmi, haswa kwa upande wa
upinzani kwa sababu ya heshima baina ya vyama husika, angalau baadhi ya
viongozi wamekuwa wazi na kueleza kwamba suala hilo lipo hata kama
halijatangazwa.
Kiongozi wa kwanza wa kisiasa kutoa kauli baada ya hatua ya
CHADEMA kumvua Zitto na Kitila vyeo vyao vyote vya kisiasa walivyokuwa navyo
ndani ya chama chao alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Akiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii, Mwigulu
alieleza kwamba kilichomkuta Zitto na Kitila ni matunda ya kuwemo katika chama
ambacho hakiendani na kaliba yao kwa sasa.
“Kwenye CHADEMA, wale wote wenye akili wako nje ya uzio wa
chemichemi ya mawazo. Mfano ni bungeni, wana CHADEMA waliowahi kufundisha
vyuoni hawapewi hata unaibu waziri kivuli kwa kuwa wanatumia zaidi akili badala
ya nguvu.
“Lakini, walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na sifuri
ndiyo majembe ya chama wanaopewa fursa zote kwa kuwa wao badala ya kutumia
akili wanatumia nguvu na mabavu.
“Nawafahamu Zitto na Kitila tangu nikiwa Chuo Kikuu na
nawajua kama watu mahiri wanaoweza kutoa mchango popote,” aliandika Mwigulu.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Mwigulu ni tofauti kwa kiasi
kikubwa na michango yake bungeni kila anapokosoa hotuba ya bajeti kutoka kwa
Wizara (kivuli) ya Fedha inayoongozwa na Zitto, akiamini imekuwa ikifanywa bila
umahiri wa kutosha.
Katika mazungumzo na gazeti moja la wiki hapa Nchini , Mwigulu
alisema “Sisi hatuna tatizo na Zitto. CCM ni chama cha Watanzania wote
kisichobagua watu kwa kutumia dhana za ukanda, udini wala ukabila.
Akitaka kuja, anakaribishwa kwa mikono miwili,” alisema
Mwigulu.
Kwa upande wa CUF, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius
Mtatiro, alisema wanafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea ndani ya CHADEMA
kwa vile ni chama mwenza katika upinzani na lolote linalotokea litakuwa na
athari katika ulingo wa kisiasa hapa nchini.
“Sitakuwa nasema ukweli kama nikisema CUF haimuhitaji Zitto,
Kitila au mwanasiasa yeyote mahiri kutoka chama chochote cha siasa hapa nchini.
Hata hivyo, si vizuri pia kwangu kusema tunamtaka mwanachama
wa chama kingine maana hilo linaweza kumaanisha tunachochea machafuko,” alisema
Mtatiro.
Hata hivyo, Habari24 inafahamu kwamba baadhi ya viongozi wa
juu wa CUF walikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kutafuta mawasiliano na Zitto
mara baada ya kuvuja kwa taarifa za mwanasiasa huyo kuvuliwa madaraka.
Mmoja wa viongozi wa juu wa CUF aliyezungumza na gazeti moja
la wiki kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema kama Zitto atahamia
katika chama chao, watakuwa wamepata kitu kimoja tu ambacho walikuwa wakikikosa
kwa muda mwingi.
“Unajua CUF Zanzibar wana Maalim Seif. Watu wanapenda sana
chama chao lakini pia wana mtu ambaye wanampenda na anakiwakilisha vizuri.
Mwenyekiti (Profesa Ibrahim Lipumba), amefanya kazi nzuri lakini haonekani kama
anaweza kuongeza idadi ya wanachama na wapenzi wa CUF. Hana ule mvuto kama wa
Maalim au alionao Zitto.
“Tunachohitaji ni mtu mmoja ambaye anaweza kuleta wanachama
wapya na msukumo mpya kwenye chama.
“Bila shaka, Zitto anaweza kuleta hilo na ndiyo maana
atakaribishwa kwa mikono miwili. Hata kama atatoa masharti ya kupewa cheo
fulani, hilo litawezekana pia,” alisema kiongozi huyo.
Akizungumzia suala la Zitto, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,
James Mbatia, alisema binafsi hawezi kuwa na tatizo iwapo mwanasiasa huyo
ataamua kuhamia kwenye chama chake ingawa alisema hajafanya mazungumzo na
mbunge mwenzake huyo kuhusu kuhamia chama chake.
Mimi kama James, sijazungumza na Zitto kumshawishi ahamie
NCCR. Hata hivyo, NCCR si James Mbatia, ni taasisi ambayo ina watu wengi. Kama
umesikia kuwa chama changu kinamtaka basi inawezekana juhudi hizo akawa
amefanya mtu mwingine lakini si mimi,” alisema.
Kama ilivyo CHADEMA kwa sasa, NCCR kiliwahi kuwa chama
kikuu cha upinzani hapa nchini lakini kikakumbwa na migogoro iliyosababisha
kushuka umaarufu wake ingawa sasa Mbatia anakijenga upya.
Mbatia alizungumzia pia mgogoro wa CHADEMA na kusema
kutokana na uzoefu wa NCCR, anaamini kwamba namna pekee ya kushughulika na
migogoro ni kuzungumzia kuhusu hoja na si watu binafsi na badala ya kutumia
sana Katiba na sheria, viongozi watumie zaidi hekima na busara.
“Migogoro inaweza ikakijenga chama kama watu wataichukulia
kwa njia chanya. Kama unapokea vibaya kutofautiana, lazima kutakuwa na
matatizo. Jambo la msingi kwa CHADEMA kwa sasa ni kujibu hoja zilizotolewa na
Zitto na si kumshughulikia yeye na mwenzake,” alisema Mbatia.
Hoja ya Zitto kuhamia NCCR inachochewa pia na ukweli kwamba
ndiyo chama chenye nguvu zaidi mkoani Kigoma anakotoka kwa sasa na tayari
baadhi ya maswahiba wake wa kisiasa kama Mbunge wa Kigoma Kusini, David
Kafulila, wamehamia huko wakitokea CHADEMA.
Kamati Kuu CHADEMA
Taarifa za ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA zimedai kwamba kambi ya Zitto na Kitila ilimtuhumu mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, Josephine, kuwa ndiye aliyesambaza ulioitwa Waraka wa Siri –ambao pamoja na mambo mengine ulidai kuwa mbunge huyo anapokea fedha kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na kuzihifadhi katika akaunti zake za nje ya nchi.
Habari24 ilimeelezwa kwamba Zitto ndiye aliyetoa madai hayo
kuhusu Josephine ambaye katika siku za karibuni amekuwa miongoni mwa
wachangiaji maarufu wa masuala ya CHADEMA katika mitandao ya kijamii.
Mpaka sasa haijulikani ni nani haswa aliyeusambaza waraka
huo lakini malamala mwandishi blogs huu aliushuhudia walaka huo kwenye blogs ya
kiongozi wa chadema ambaye jina tunalihifadhi, uliosababisha Zitto aende
kushitaki polisi, lakini inajulikana kuwa Slaa ni miongoni mwa waliovutiwa na
maudhui yake kiasi cha ku-like waraka huo mtandaoni.
CHADEMA kimekana kuhusika na waraka huo lakini malalamiko ya
Zitto yalikuwa kuhusu hatua ya bosi wake (Slaa) ‘kuupenda’ waraka huo wakati
ulikuwa ukimkashifu na kumvunjia heshima mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa
chama chao.
Blogs hii linaarifiwa katika kikao hicho, Mwanasheria Mkuu
wa CHADEMA, Tundu Lissu pamoja Mwenyekiti wa chama hicho katika mikoa ya Kanda
ya Kusini, Matare Matiko, ndiyo walioongoza mashambulizi dhidi ya Zitto kwenye
kikao hicho huku Msafiri Mtemelwa, akiongoza katika watetezi wa Zitto.
Ni Lissu ambaye baada ya Zitto na Kitila kutoa hoja ya
kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama – aliibua hoja ya kutaka wasikubaliwe
kujivua wenyewe bali wavuliwe na chama na watakiwe kujieleza kwa nini
wasifukuzwe chama
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na mwandiashi
wa blogs walisema Kama nilivyotangulia kusema kuwa Watanzania wapenda mageuzi
na nchi yao hawawezi kukubali CHADEMA ikafa kibudu kwa sababu tu ya kuwalea
wasaliti wanaochuma rushwa kwa ajili ya matumbo yao, ukweli sasa
umedhihiri, wasaliti wasakwe popote na kutoswa.
Watu wamekufa, wamemwaga damu,
wamebaki vilema kwa kipigo cha mitutu ya dola wakati wakiimarisha CHADEMA, nani
anaweza leo kuendelea kuwaonea haya wala rushwa na walevi wa madaraka eti
wakisambaratishe chama CCM ipumue
No comments:
Post a Comment