Na Karoli Vinsent
Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeingia kwenye kashfa ya
ufisadi wa Sh2.3 mil za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali baada ya viongozi wa
CCM wilaya hiyo kuitaja waziwazi kwamba wanahusika katika kashfa hiyo ilitokea
mwaka 2011/12.
ENDELEA HAPO------
ENDELEA HAPO------
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo
alimweleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea wilaya hiyo jana
kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ni moja ya kikwazo kitakachosababisha CCM iwe na
hali ngumu wilayani humu kutokana na kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa
ufisadi huo.
Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo
zilichakachuliwa kwa ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na kwamba
mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.
Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri hiyo kwani
madiwani sita walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM kwa tuhuma za
kushirikiana na watendaji katika kutafuna fedha hizo
Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa karibnu na
kwamba lazima zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani,
Vitendo vya ufisadi ndani ya halmashauri nyingi hapa nchini
vimekuwa sana huku Mamlaka zikiwa zinayafumbia macho vitendo hivi.hii imekuja
baada ya ripoto za mkaguzi wa fedha CAG kuonyesha ufisadi katika halmashauri
nyingi hapa nchini huku zengine zikiwa zimepewa hati chafu kutokana na ufisadi
unaoendelea katika halmashauri hizo lakini jambo la kushangaza viongozi ambao
wanapelekea ufisadi huwa wanaamishwa kazi kutoka katika halmashauri moja kwenda
nyingine,
Duru za kisiasa zinasema kitendo cha
kuwahamisha viongozi wanaopelekea ufisadi ni kuficha uhovu na pia ni dalili za
kulinda mafisadi hao
No comments:
Post a Comment