KAIMU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI MOSENA JOHN NYAMBABE AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI MAPEMA LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Chama cha NCCR mageuzi kimetangaza rasmi kuwa kila mwaka ifikapo tarehe 12 ya mwezi wa 11 ambapo dk sengondo mvungi alifariki itakuwa siku ya kumkumbuka ambapo wamesema kuwa watafanya mambo mengi ya kuikumbuka siku hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam kaimu katibu mkuu wa chama hico MOSENA NYAMBABE amesema kuwa chama hicho kimeamua kuifanya siku hiyo kuwa siku maalum ya kumkumbuka dk MVUNGI ambapo chama hicho kwa kushirikiana na watanzania wote wataendesha mihadhara ya kujadili kazi alizozifanya dk MVUNGI pamoja na kujadili mambo mbalimbali ambayo aliyasimamia ikiwemo swala la katiba na utetezi wa haki za binadamu.
Aidha amesema kuwa chama hicho kinaahidi kumuenzi dk MVUNGI kwa yale yote aliyokuwa akiyatenda mazuzi na yenye maslahi kwa taifa kwa ujumla.
Aidha katika hatua nyingine chama hicho kitafanya sala maalumu tarehe 14 ya mwezi huu wa 12 katika kanisa la mt JOSEPH jjini dar es salaam kwa ajili ya kumwombea marehemu dk MVUNGI.
No comments:
Post a Comment