...Kampuni inayoleta pamoja ubunifu na malengo kwa kuwa pekee
kuzinduliwa bila jina.
Dar es salaam, Desemba 11, 2013 – Muigizaji wa
vichekesho kwenye kundi la Mizengwe Hemedi Khalida maarufu kama Mkwere
ameangukiwa na neema ya ubalozi wa kuhamasisha upatikanaji wa jina la
kampuni ya simu iliyoziduliwa bila jina. Kampeni hiyo itafanyika kupitia simu
na mitandao mbalimbali ambapo wananchi wanatakiwa kuipatia jina kampuni hiyo.
Mbali na hayo Mkwere atapata nafasi ya kupita mitaa mbalimbali akiwahimiza
wananchi kupiga kura.
ENDELEA HAPO CHINI-----------
Sekta ya mawasiliano
ya simu Tanzania na Afrika Mashariki imepata matumaini mapya kufuatia kuingia
kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu, yenye kuamini jamii, na yenye
ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila jina.
Pamoja na ahadi yake
ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao wa simu, kampuni hiyo
mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya kiubunifu inayotambulika kwa
jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu
kwa lengo la kuipa fursa Afrika Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa
kupiga kura.
Hii ni kampuni ya
kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na haigopi kuamini watu,
na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu kufanya hivyo. Hakuna kampuni
yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya
kusisimua kabla ya jina kuwekwa hadharani.
“Tupe Jina” ni kampeni itafanyika
kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa
facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua majina
ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.
Mshirki anaweza
kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina kwa njia
ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina
analopendekeza kwenda namba 15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini
majina yote na itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya
kipekee na yenye ubunifu.
Baada ya hapo
Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora moja ambalo
hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya mawasiliano ya simu ambayo
daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu
ambaye atakuwa amechagua jina ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia
muda wa bure wa kupiga simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Zawadi zingine
zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za kiganjani (tablets) kwa
washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”.
Kutokana na wataalam
kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka asilimia 4 hivi sasa
hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano ina nafasi kubwa ya katika
ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na kampuni hii mpya ya mawasiliano ya
inawakilisha sura ya kasi hii kubwa ya ukuaji.
Tanzania inabaki kuwa
ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya asilimia 50 kufikia
Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu nchini humo ni chini ya
wastani kwa nchi za Afrika.
Hii kampuni mpya ya
simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wateja wake
kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa watu wa Tanzania katika sekta ya afya
na hasa katika tiba za kimtandao na vituo vya elimu ya masafa.
Hii tafsiri yake ni
kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha Afrika Mpya
kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na zawadi bora ambayo
kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza sekta ya afya.
Baada ya kampeni ya
“Tupe Jina” wananchi wa Tanzania watapata nafasi ya kupeleka namba zao
wanazopendekeza kabla ya kutangazwa na kuwekwa hadharani kwa jina la kampuni.
-Mwisho-
No comments:
Post a Comment